Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
wananchi wa Kitongoji cha Wangamiko Kata ya Malangali Wilayani
Wanging’ombe mkoani Njombe jana wakati alipotembelea mradi wa ufugaji wa
nyuki unaoendeshwa na jumuiya ya wa Wazazi ya CCM wilaya ya
Wanging’ombe mkoani humo, Pia Kinana aliridhishwa na shughuli za
maendeleo zinazofanywa na vijana wa kitongoji hicho na kuamua kuwapatia
jumla ya shilingi milioni 10 ili kujiendeleza katika shughuli zao za
miradi ya kiuchumi , pia aliwapatia jezi za michezo seti mbili na
mipira 10 kwa ajili ya kuunda timu zao za mpira wa miguu.
Katika hatua nyingine alikipa kitongoji hicho mifuko 25 ya saruji ili
kumalizia ofisi yao ya CCM, Katika maombi yao wananchi hao wamemuomba
Katibu Mkuu wa (CCM)
kulifikisha ombi lao kwa TAMISEMI ili kitongoji hicho kipandishwe na
kuwa na hadhi ya kijiji
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abulrahman Kinana akizindua mradi wa ufugaji nyuki
katika kitongoji cha Wangamilo kwa kuutundika mzinga wa nyuki kwenye
mti, mradi huo unaedeshwa na jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya
Wanging’ombe, Kinana aliipatia jumuiya hiyo mizinga mingine 25 ili
kuendeleza mradi wao
Umati wa wananchi ukinyanyua mikono juu kuashiria kufurahishwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana hayupo pichani
Katibu
wa Itikadi , Siasa na Uenezi CCM Nape Nnauye akimpiga picha Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana wakati alipokuwa akihutubia katika
kitongoji cha Wangamiko
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahmani Kinana na Katibu Wa Itikadi , Siasa na Uenezi
Nape Nnauye waakichanganya Mchanga na saruji wakati walipotembelea na
kukagua ujenzi wa zahanati ya Samaria Wangingombe
Hapa
akikagua ujenzi wa Zatanati ya Samaria na kuuliza maswali kadhaa, hata
hivyo aliridhishwa kwa mjinsi wananchi wanavhoshiriki shughuli za
maendeleo katika kata hiyo.
Hapa
akiangalia unga wa mahindi unaotengenezwa na Kiwanada cha Mbomole
Investiment Co. Cha Malangali Wanging’ombe wakati alipotembelea
maonyesho ya wajasiriamali na wakulima wilayani humo
Hapa akizungumza na wananchama wa shina moja wapo katika kata ya Iwawa Makete shina hili linaongozwa na mzee Danke Sanga
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki zoezi la kufyatua
tofari wakati alipotembelea ujenzi wa zahanati ya Samaria akiwa njiani
kuelekea Malangali Wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.
0 comments:
Chapisha Maoni