Searching...
Ijumaa, 21 Juni 2013

KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU MBINGA ALIA KUHUJUMIWA NA VIONGOZI WA WILAYA HIYO

 Katibu wa Chama cha walimu(CWT) Tanzania tawi la Mbinga Samwel Mhaiki akifafanua jambo alipokuwa akijibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo ya matumizi mabasya ya ofisi na kuwa kinara wa migogoro ya mara kwa mara na pia kuwachonganisha Walimu wa wilaya hiyo na Serikali na kuendesha hujuma kwa Afisa elimu ya msingi wa wilaya hiyo Mathias Mkiali
 Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la saba kutoka kata ya Kigonsera Kilayani Mbinga -Ruvuma walioko katika makambi maalum ya kujisomea yene lengo la kuongeza taaluma katika wilaya hiyo wakiwa katika mstari wa kusubiri chakula cha  mchana kama walivyokutwa na mpiga picha wetu jana.
 Mratibu elimu kata ya Kigonsera katika Wilaya ya Mbinga  Sebastian  Lupogo wa pili kushoto na afisa elimu ya msingi wa wilaya hiyo Mathias Mkali wakiangalia chakula kinachotumika na wanafunzi walioko katika makambi maalum ya kujisomea kabla ya kufanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi miezi miwili ijayo.
-------------------------
Na Muhidin Amri-Mbinga
KATIBU wa Chama cha walimu(CWT)Wilayani hapa Samwel Mhaiki amekanusha vikali tuhuma zilizoelekezwa  dhidi yake na Mkuu wa Wilaya hiyo Senyi Ngaga kuwa yeye ni kinara wa migogoro ya muda mrefu iliyopo kati ya baadhi ya watumishi wa Idara ya elimu na Afisa elimu ya msingi Mathias Mkali badala yake amemshushia lawama Mkuu huyo wa Wilaya kuwa yeye ndiyo tatizo kubwa la migogoro hiyo kufuatia kushindwa kwake kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaoendelea  kumpiga majungu na kumfanyia fitina Mkali.
Aidha ameeleza kuwa yeye amekuwa akijitahidi sana kutaka kufanyika vikao vya mara kwa mara kutafuta njia sahihi ya kuitolea aibu wilaya ya Mbinga kutokana na matokeo mabaya ya mitihani ya kumaliza elimu ya  Msingi lakini viongozi wa wilaya hiyo hawampi  ushirikiano wa kutosha  kwa kile kilichoelezwa  baadhi yao wanamaslahi binafsi.
Mhaiki alifafanua kuwa,hata mgogoro wa muda mrefu uliopo kati ya Afisa elimu ya msingi Mathias Mkali na baadhi ya watumishi wa Idara ya elimu na kigogo mmoja wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambaye kwa sasa amepata uhamisho umechangiwa kwa kiasi kikubwa na maslahi binafsi na kuwaomba viongozi  hao  kutomtafuta mchawi katika kushuka kwa taaluma wilayani Mbinga badala yake wafahamu adui namba moja wa elimu ni mgogoro huo ambao unachangia kutokuwepo kwa maelewano mazuri kati ya watumishi wa idara hiyo  baadhi ya vigogo wa Halmashauri ya wilaya Mbinga na kushauri njia pekee ni kuungana pamoja  na kuangalia mapungufu yaliopo ambayo yamekuwa kama donda  la muda mrefu  ili yaweze kufanyiwa kazi.

"hizi tuhuma dhidi yangu ni kunionea bure mimi siusiki kabisa wao wenyewe ndiyo tatizo la elimu katika wilaya yetu kila mara naandika barua ya kuomba vikao lakini hawanijali na kuniona ni  mbabaishaji na hata kufikia kuniita adui wa kwanza katika elimu hayo sio sahihi hata kidogo"alisema Mhaiki.

               PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DEMASHO BLOG

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!