Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akiwasili viwanja vya kata ya kimandolu jioni hii ya tar.7/06/2013 kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani kata ya kimandolu kwa tiketi ya CCM Bi,Edna Jonathan Saul

Kada wa CCM Bi.Juliana shonza akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za udiwani.Bi.Juliana shonza amewaomba wa Kimandolu kumpigia kura Bi.Edna Saul kwa sababu ni mpiganaji na Mwanamaendeleo ya kweli tena Mwanamke.Bi.Juliana amesema ni upuuzi kwa mwananchi wa Arusha kukiunga mkono CHADEMA ,amedai CHADEMA kina sera ya kurudisha maendeleo nyuma na sio mbele.Amesisitiza kazi ya chadema ni kuandamanisha na kuwacheleweshea muda wananchi,Ametoa mfano wa uchaguzi mdogo unaofanyika sasa Arusha ni kwasababu ya CHADEMA.Wamefukuza madiwani kwa matakwa ya watu wa chache na sio wananchi waliowachagua.Naomba wana Kimandolu mjitokeze kupiga kura kwa mgombea wa CCM ili kuleta maendeleo kwa jiji la ARUSHA.

Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Mh.Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea udiwani kata ya Kimandolu jijini Arusha Bi.Edna Jonathan Saul.Mwigulu nchemba amewaomba wana-Kimandolu kufanya chaguo sahihi  na lakimaendeleo kwa kumchagua mgombea wa CCM.Amesisitiza Arusha kwa sasa ni kama haina Mbunge kwa sababu Mbunge wa Arusha kazi yake ni kupanga uvunjifu wa amani na kuandamanisha watu iliapate sifa za kijinga.Amewauliza wanaarusha ni maendeleo gani aliyoleta lema?Ameuliza marangapi wamemsikia Lema akiongeza kwenye bunge?.Hivyo basi hakuna haja ya kukiunga mkono chama cha CHADEMA."Naomba wana CCM mfanye kazi ya kuwa mabalozi kwenye kampeni hizi.jitokezeni kupiga kura na mhakikishe mnawafungua macho na wenzenu kwamba maendeleo hayaletwi kwa maandamano au kusababisha vifo vya watanzania wasio na hatia.

Bi.Juliana Shonza akihutubia wananchi kata ya kimandolu jioni hii

Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu nchemba akihutubia mamia ya wakazi wa jiji la Arusha  kata ya Kimandolu kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.Mh.Mwigulu nchemba amesisitiza kudumisha Amani ndani ya jiji la Arusha,Amewasihi wanaarusha kuacha kushabikia vyama vinavyofurahia na kuhubiri vurugu siku zote."Wanaarusha kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani si kubadirisha serikali,Serikali itabaki ileile ya CCM na sera zitabaki zilezile za CCM,tunachokifanya hapa ni kuongeza nguvu ilikurejesha heshima ya chama cha mapinduzi na jiji la Arusha.Kumekuwa na sifa mbaya kwamba Arusha sikuhizi hakuana amani,daladala zinasurutishwa kugoma ilimradi tu mbunge wa CHADEMA Godbless Lema asikike kwamba leo ameleta vurugu.WanaArusha sifa za kijinga zimepitw ana wakati,fanyeni chaguo sahihi kwa kumchagua Bi.Edna Saul kuwa diwani wa CCM kata ya kimandolu

Hapa Mh.mwigulu Nchemba alikuwa anahoji CHADEMA wameleta maendeleo gani hapa Arusha?Kubwa ni vurugu na kukosesha Amani jiji la Arusha,Hivyo ikataeni CHADEMA kama ukoma

Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Mboye alikuwepo kwenye mkutanoi huo wa kampeni za udiwani kata ya Kimandolu.Amesisitiza amechoshwa na kuwa mratibu wa maandamano ya vurugu jiji la Arusha.Ameshapoteza muda wake mwigi sana kwasababu ya CHADEMA.Hivyo ni bora kuichagua CCM chama makini na chenye Amani kuliko kuipa kura CHADEMA .Ametoa rola tano za mabomba ya maji kwaajilia ya maendeleo ya kata ya Kimandolu

Hapa Mh.Mwigulu nchemba amerejea wito wake kwa wakazi wa Arusha kwamba amani ni tunu ya Taifa tuilinde na kuiheshimu.Vita sijambo la kukimbilia wala kulifurahia,Siasa si kuuana au kuumizana kama wanyama.Amesisitiza kuwa kampeni za uchaguzi ni lazima ziwe na misingi ya amani kama utamaduni wa watanzani.Amemuonesha kija Musa aliyejeruhiwa kwenye uchaguzi wa IGUNGA.Amesema kunavyama vinaposhindwa kujitetea jukwaani wanakimbilia kuvunja amani na kujeruhi watu ili wapate misaada toka kwa ndugu zao nje ya nchi.

Sehemu ya mamia ya watu waliojitokeza kwenye kampeni za uchaguzi wa udiwani Kata ya Kimandolu jijini Arusha

Mh.Mwigulu Nchemba akimuonesha kijana Musa mbele ya wananchi kwamba haya ndio matunda ya vyama vya maandamano.

Bi.Edna Jonatahan Saul akihutubia wanachama wa CCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni kata ya Kimandolu jioni hii.Bi.Edna Jonathan Saul ameomba wana CCM na wakazi wa kata ya Kimandolu kumpigia kura za Ndio kwenye uchaguzi huu mdogo wa Udiwani.Amesisitiza kuwa yeye ni mfuatiliaji sana wa maendeleo na ni mzawa wa kata hiyo.Amesisitiza wana CCM wachague kurejesha amani jiji la Arusha,kumpigia kura Edna ni kujiongezea nafasi ya kupata maendeleo makubwa ndani ya kata hii.

Bi.Edna Jonathan Saul


Sehemu ya mkutano wa CCM kata ya kimandolu jijini Arusha

Bi.Edna jonatahan Saul Mgombea wa udiwani kata ya kimandolu kwa tiketi ya CCM

Kada wa CCM Mtela Mwampamba akisistiza kuwa wana-Kimandolu wampigie kura Bi.Edna Saul ilikuachana na vurugu za kila siku ndani ya jiji la Arusha.Pia ameomba wanachadema wamfundishe Mbunge wao Lema maana ya Mahusiano,.kwa sababu lema hajui mahusian ya Amani na maendeleo ya nchi(Picha zotena HM)