Searching...
Ijumaa, 21 Juni 2013

JUAN MATA NA RAMIRES KUBAKI DARAJANI ASEMA MORINYO.

Going nowhere: Chelsea see Mata as a key cog not a spare partJUAN MATA AKISHANGILIA MOJA YA MAGOLI YAKE CHELSEA.
Kocha mpya wa chelsea ambaye amerejea kuifundisha klabu hiyo kwa mara ya pili amesema mhispania huyo JUAN MATA ni mmoja kati ya wachezaji anaowahitaji kufanya naye kazi msimu ujao na kuhutimisha uvumi uliokuwa umezagaa kwamba mshambuliaji huyo anatarajiwa kutua Barcelona na MORINYO ameziita tetesi hiso kuwa uzushi wa kipuuzi.
Chelsea's new manager Jose Mourinho
JOSE MOURINHO.
  Jose Mourinho amekaririwa na mtandao wa klabu hiyo akisema yupo tayari kumsainisha Juan Mata mkataba mnono na mrefu wa miaka mitano
Taarifa zaidi zinasema huenda Demba Ba na Fernando Torres wakatimka klabuni hapo kwani hawapo kwenye orodha ya Mourinho

Ramires celebrates Chelsea's opener against Wigan
RAMIRES.
Mchezaji mwingine anayetarajiwa kusalia klabuni hapo ni mbrazili kiungo Ramires baada ya kuweka wazi kwamba Mourinho amempigia simu na kumjulisha kwamba ataendelea kusalia klabuni hapo msimu ujao.
Ramires ambaye ameondolewa na kocha wa brazil Luiz Felipe Scolari kwenye orodha ya kikosi cha Brazil kinachoendelea na mashindano ya kombe la confederations amesema kwa sasa anaendelea na mapumziko huko nyumbani kwao Brazil.
 
 “ninayo furaha kubwa sana kufanya kazii na  Mourinho.
“ amenipigia siku chache zilizopita,kitu ambacho kilinishangaza na kunifurahisha sana
“ameniambia mambo mazuri  mengi sana ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba alijaribu kunisajili kwa kipindi chote akiwa Inter Milan na Real Madrid kipindi hicho nikiwa Benfica.
“Mourinho ameniambia anayofuraha kubwa sana kufanya kazi na mimi Chelsea...kwakweli ninayo furaha sana...Alisema Ramires.


0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!