Arsenal sasa wameingia kwenye orodha ya
vilabu vya ligi kuu England vinavyotumia fedha nyingi kusajili baada ya
kufikia hatua za mwisho za kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo
Higuain ambaye atawagharimu kiasi cha paundi millioni 50.
WAYNE ROONY AKIWA KAZINI NA TIMU YA TAIFA ENGLAND DHIDI YA BRAZIL.
wakati bilionea huyo wa Arsenal
Alisher Usmanov akimsainisha Higuan amemtaka kocha wa klabu hiyo Arsene
Wenger kutoa kitita kingine ili kuipata saini ya mshambuliaji wa
Manchester United Wayne
Rooney ambaye ameshaweka wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo,ambapo tayari taarifa zinasema kama arsenal watachelewa kumsainisha huenda akatua Chelsea kwani ni mmoja kati wachezaji wanaotakiwa na Mourinyo.
Mapema mwezi huu mkurugenzi wa klabu
hiyo ya Arsenal Ivan Gazidis alisema kwa sasa klabu ipo katika hali
nzuri kununua wachezaji wenye majina makubwa kama zinavyofanya
CHELSEA,MAN U na MAN CITY.
THIAGO ALCANTARA
Inasemekana ujio wa mchezaji THIAGO ALCANTARA kutoka Barcelona ni moja ya sababu inayomkimbiza Roony Manchester United.
0 comments:
Chapisha Maoni