CARLOS TEVEZ.
Hayawi hayawi sasa yanaanza kukua,baada ya tetesi nyingi kuhusu mchezaji wa Manchester City Muargentina CARLOS TEVEZ kuhusishwa kuhamia vilabu mbalimbali hatimaye leo asubuhi taarifa rasmi kutoka Man City zinasema klabu hiyo imekubaliana na klabu ya Juventus ya Italia kumuuza mshambuliaji huyo kwa ada ya paundi milioni12.
Mchezaji huyo anatarajiwa kutua italia jumatano kwaajili ya vipimo pamoja na makubaliano mengine ya mkataba wa miaka mitatu ya kukipiga na vijukuu hivyo vya kibibi kizee cha Turin.
Taarifa kutoka Manchester City zinasema kumuuza Tevez ukichanganya mshahara na marupurupu aliyokuwa akichukua klabuni hapo wataweza kuokoa kiasi cha paundi milioni 27 hadi alipokuwa amalize mkataba wake klabuni hapo.
vilabu hivyo viwili vimeweza kufikia makubaliano hayo jana jumanne kwenye kikao kilichofanyika jijini London.
Carlos Tevez alikuwa amesaini mkataba wa miaka mitano na Man City alipohamia klabu hiyo mwaka 2009 akitokea klabu pinzani Manchester City baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati ya msukuma kandanda huyo wa Argentina na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo babu Sir Alex Ferguson.
Carlos Tervez ameichezea klabu ya Manchester City mechi 148 na kuifungia jumla ya magoli 74,japo mahusiano yake na kocha wa zamani wa klabu hiyo Roberto Mancini haukuwa mzuri baada ya kuondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa klabu hiyo mwaka 2011 baada ya kugoma kuingia uwanjani wakati wa mechi ya klabu bingwa ulaya kati ya City na Baryen Munich ya ujerumani
0 comments:
Chapisha Maoni