Hatimaye mshambuliaji wa chelsea aliyenunuliwa kwa kitita kikubwa cha fedha kutoka Liverpool Fernando Torres ameripotiwa kutaka kutimkia Hispania ili kukipiga na klabu ya Barcelona msimu ujao.
kurejea kwa kocha mreno mwenye falsafa ya kupenda washambuliaji wanaotumia nguvu alikaririwa akisema angependa kuendelea kufanya kazi na mshambuliaji huyo lakini akaongeza kwamba hiyo itategemea na maamuzi ya mchezaji mwenyewe kuhusu matakwa yake ya baadae.
Chelsea imetangaza kwamba thamani ya Torres ni paundi milioni 50 lakini Barcelona wao wamesema wapo tayari kutoa paundi milioni 17 ili kumnyakua mchezaji huyo ambaye kwa sasa yupo na timu yake ya taifa katika kombe la federation....Habari hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Hispania.
0 comments:
Chapisha Maoni