RAIS JACKOB ZUMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU HALI YA MZEE MANDELA.
Hali ya afya ya Rais wa zamani wa Afrika
Kusini Mzee Nelson Mandela imeendelea kudhorota katika kipindi cha saa ishirini
na nne zilizopita.
Akizungumza na vyombo vya habari vya
nchi hiyo rais Zuma amesema kwa sasa
madaktari wanaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanaokoa uhai wa Mzee
Mandela,lakini akakataa kutoa maelezo zaidi ya madaktari.
Raisi huyo wa kwanza mweusi wa
afrika kusini mwenye umri wa miaka 94 alikimbizwa hosiptalini Pretoria mapema
mwezi huu ikiwa ni mara ya tatu kwa mwaka huu ambapo taarifa zinasema
anasumbuliwa na matatizo ya mapafu na mfumo wa upumuaji.
Jana jumapili rais Zuma alitangaza
kwamba hali ya Mzee Mandela sio nzuri baada ya kumtembelea hosptalini ambapo
alimkuta akiwa amelala lakini aliweza kuongea na mke wake pamoja na timu nzima
ya madaktari wanaomtibu.
"sisi sote wananchi wa afrika kusini ni lazima
tukubali kwamba Madiba(jina la mzee Nelson Mandela la ukoo) kwa sasa ni
mzee,afya yake sio nzuri kwahiyo mimi nafikiri kitu tunachopaswa kukifanya ni
kumuombea" alisema raisi Jackob Zuma.
0 comments:
Chapisha Maoni