Siku ya ijumaa tarehe 31 mwezi wa tano
mwaka huu, kwa mshangao wa wengi yalibandikwa matangazo kwenye hospitali
ya KCMC kuwa kuanzia jumamosi tarehe 01 june, huduma za matibabu kcmc
zimepanda kwa viwango tofauti kati ya asilimia 450-1000. Hebu jionee
mwenyewe hapa chini:
Kumuona daktari TOKA Tsh2,500/= HADI Tsh10,000/=
Cesarean/SECTION ("Oparesheni ya kumtoa mtoto tumboni") TOKA Tsh100,000/= HADI Tsh520,000/=
Minor Operesheni Toka Tsh100,000/= HADI Tsh450,000/=
Kwa major operations Tsh650,000/= (kwa major operations kama laparatomy au "kufungua tumbo" kwa lugha rahisi)
Kwa extensive surgeries ni Tsh1,600,000/= (Kama craniotomy/burr hole exploration kwa lugha rahisi "kufungua kichwa")
Kitanda Toka Tsh5,000/= HADI Tsh35,000/= kwa siku
Operesheni za kutumia camera (LAPARASCOPIC SURGERIES) Kutoka Tsh100,000/= HADI Tsh800,000/=

Wagonjwa waliokuwa wamelazwa wanawalazimisha madaktari wawaruhusu kwa sababu wanasema gharama ni kubwa mno, hawaziwezi na pia kuna wagonjwa wengi wametoroka wodini kukimbia gharama kubwa. Mbaya zaidi tangazo hilo limetolewa ghafla, na bei mpya zimeanza kutumika ghafla bila kutoa nafasi kwa wagonjwa kujiandaa na gharama mpya hizo kama ilivyozoeleka kukiwa na ongezeko.
Mimi tatizo langu moja tu, hivi ile public-private partnership kati ya serikali na hospitali hii imekufa au? je serikali imeacha kuleta fungu kama ilivyokuwa inafanya na kuwezesha huduma hizi kuwa nafuu kidogo kwa watanzania? Kama jibu ni ndiyo, mbona hatujaambiwa? kama jibu ni hapana, kwa nini ongezeko kubwa hivi tena kwa ghafla??
CHANZO:JAMII FORUM
0 comments:
Chapisha Maoni