ANGALIA PICHA ZA GARI ALIYOPATA NAYO AJARI MASELE CHA POMBE
Masele cha
pombe jana tarehe 14 mchana zilisambaa habari kwamba amepata ajali ya gari na
amefariki dunia. Jibu sio kweli na ishu nzima ni kwamba alipata ajali akiwa
barabara ya 14 Tanga baada ya kumgonga mtu mmoja. Akiwa katika harakati za
kupaki gari na kushuka, wananchi walianza kumshambuli kwa mawe ndipo hapo
Masele alipojaribu kuokoa maisha yake kwa kuwasha gari na kuanza kukimbia,
bahati mbaya baada ya hapo akamgonga mtu mwingine bahati mbaya ndipo watu
wakalikuta gari lake na kuanza kulipiga mawe na wengine kuchoma visu matairi ya
gali hilo. Chanzo kilichotutumia habari hii kinaendelea kusema kwamba hadi
Masele mwenyewe ameibiwa hela zake pamoja na simu yake ya mkononi. Lakini hivi
sasa yupo mzima kabisa