Msafara
wa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja ukiwasili katika
viwanja vya Chuo cha ufundi Ruanda Jijini Mbeya kwa ajili ya kuwatunuku
nishani Maaskari wa Jeshi la Magereza.
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akikagua Gwaride maalum
lililoandaliwa na maaskari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake mara
baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuwatunuku nishani
Maaskari.
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akipokea Salamu za heshima
kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya.
Baadhi
ya Maaskari wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Kamishina Jenerali
wa Magereza CGP John C. Minja (ambaye haonekani pichani) wakati wa
hafla ya kuwatunuku nishani.
Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira Rungwe wakitumbuiza katika Sherehe hizo.
Baadhi ya Maaskari wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na maofisa wakifuatilia kwa umakini Sherehe za kutunuku nishani.
Baadhi ya Maaskari wakisubiri kutunukiwa nishani kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja.
SACP
C. A Keenja akitaja majina 29 ya Maaskari wanaotakiwa kutunukiwa
Nishani ya Utumishi uliotukukuka Tanzania, Utumishi wa Muda Mrefu Tanzania,
Utumishi mrefu na tabia njema na Mwenge wa Uhuru daraja la nne
0 comments:
Chapisha Maoni