Searching...
Jumatano, 15 Mei 2013

WAZIRI MEMBE AKUTANA NA MABOLOZI WA NJE HAPA TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kitaifa. Katika Mkutano huo Mhe. Membe alifafanua juu ya hali ya kisiasa nchini Madagascar na Zimbabwe na kutoa taarifa za kuwasili kwa vikosi vya kulinda amani vya Tanzania huko Mashariki mwa DRC. Kuhusu masuala ya kitaifa Mhe. Membe alilitolea ufafanuzi suala la shambulio la bomu lilitokea hivi karibuni huko Arusha ambapo alisema kuwa Serikali inaendelea na uchunguzi  na kwa ujumla hali nchini ni tulivu. Wengine katika picha ni Bw. John Haule (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe.Khalfan  Juma Mpango (kulia), Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei, 2013.
Balozi Mpango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake mara baada ya Mhe. Membe kumaliza mazungumzo nao.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa pili kushoto) kwa pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) wakati alipozungumza na Mabalozi hao.
Sehemu nyingine ya Mabalozi wakati Mhe. Membe alipozungumza nao.
Mabalozi wengine wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mohammed Maharage (kushoto) akimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) alipozungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mabalozi wengine na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Picha zaidi za mkutano huo wa Mhe. Membe na Mabalozi.
Mhe. Waziri Membe akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Balozi Abdulla Ibrahim Al-Sowaidi hapa nchini baada ya kumaliza mazungumzo.
Mhe. Membe akiagana na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filiberto Sebregondi mara baada ya mazungumzo na Mabalozi hao.
Balozi wa Rwanda hapa nchini akifuatana na Mhe. Membe alipomaliza mazungumzo na Mabalozi hao.
Mhe. Membe akiasalimiana na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Alfonso Lenhardt aliyekuwepo wakati wa mkutano huo.
Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa nchini, Mhe. Francisco Montecillo Padilla mara baada ya kuzungumza na Mabalozi hao.
Mhe. Membe akizungumza na Waandishii wa Vyombo mbalimbali vya Habari juu ya mazungumzo yake  na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hao hapa nchini.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!