Searching...
Jumamosi, 4 Mei 2013

WAZIRI DK.MWINYI AZINDUA BODI MPYA YA NHIF

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdoe alipowasili kuzindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa NHIF, leo kwenye Hoteli ya Courty Yard, Sea View, Dar es Salaam. Wengine ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Regina Kikoli.
 Wakurugenzi wa NHIF, wakipiga makofi wakati Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Mwinyi alipokuwa akiingia kuzindua bodi hiyo.
Dk. Mwinyi akihutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Mchumo.
 Baadhi ya mameneja wa Mikoa wa NHIF, na maofisa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo.
 Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Mchumo (kushoto) akimshukuru Waziri, Dk. Mwinyi kwa kuzindua bodi hiyo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Humba.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa maelezo kuhusu utendaji wa mfuko huo,  Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli.
 Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Balozi Ali Mchumo akuhutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (wa nne kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya NHIF. Kutoka kushoto ni Mwanaidi Mtanda,Donnan Mmbando, Mwenyekiti Balozi Ali Mchumo, Mohammed  Hashim, Charles Kajege, Dk. Ali Mohammed na Naibu Katibu Mkuu wa wa wizara hiyo, Regina Kikoli.Waliosimama ni Mkurugenzi Mkuu, Emmanuel Humba (kulia na Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamis Mdoe.
 Waziri Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi pamoja na wakurugenzi wa NHIF.
 Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
 Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
WAZIRI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
Dk.Mwinyi akibadilishana mawazo na Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (kushoto) pamoja na Mjumbe wa bodi hiyo, Mohammed Hashim.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli 9kulia) akiagana na Balozi Ali Mchumo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.


0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!