|
`Kaimu
mganga mkuu wa serikali Dkt. Mohamed Mohamed akifungua mkutano wa
Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala leo jijini Dar es
salaam waliokutana kujadili mafanikio, changamoto na mipango mbalimbali
waliyonayo katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba za Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Paulo Mohammed akitoa ufafanuzi wa hali
halisi ya Tiba za Asili na Tiba mbadala nchini Tanzania na mpango wa
serikali wa kuendelea kuthamini huduma inayotolewa na wataalam hao
wakati wa mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba
mbadala.
Mratibu
wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO)
Rose Shija akisoma salam za mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini
Tanzania Dkt. Rufaro Chatora leo jijini Dar es salaam ambaye amepongeza
juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya
kutatua changamoto zinazowakabili wataalam wa Tiba za Asili na Tiba
mbadala.
Mtafiti
mwandamizi mkuu wa Idara ya Utafiti wa Tiba Asili kutoka Taasisi ya
Utafiti wa magonjwa ya Binadamu Hamis Masanja Malebo akitoa mada kuhusu
historia ya Tiba za Asili na uhusiano uliopo katika matumizi ya mimea
ya asili kati ya tiba za asili na tiba mbadala na tiba za kisasa katika
utengenezaji wa dawa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Sehemu
ya wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala waliohudhuria mkutano wa
Baraza la Wataalam wa tiba hiyo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati
wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
|
Jumamosi, 25 Mei 2013
Related Posts
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni