BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA KIGOMA IMEWATUNUKU WAKAZI WAWILI WA KIJIJI CHA
KATUNDU KATIKA WILAYA YA KASULU, BAADA YA WANANCHI HAO KUFANIKIWA KUWADHIBITI
MAJAMBAZI WAWILI TOKA BURUNDI NA KUMUUA MMOJA KATIKA TUKIO LA UTEKAJI WA
KUTUMIA SILAHA LILILOTOKEA WIKI MBILI ZILIZOPITA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIGOMA FRAISSER KASHAI
AKIJIANDAA KUTOA CHETI KWA MWANANCHI ALIYEKABILIANA NA MAJAMBAZI TOKA BURUNDI
NA KUMUUA NA KUCHUKUA SILAHA, KABLA YA KUANZA KWA KIKAO CHA KAMATI
YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA
AKIZUNGUMZA KABLA YA KUKABIDHI CHETI NA HUNDI YA SHILINGI
LAKI NNE, MWENYEKITI WA KAMATI HIYO AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA KIGOMA LUTEN
KANAL MSTAAFU ISSA MACHIBYA AMEWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA
DOLA ILI KUDHIBITI UHALIFU WA KUTUMIA SILAHA ULIOSHAMIRI MKOANI KIGOMA, HUKU
AFISA UHAMIAJI WA MKOA SAIDI KAMUGISHA AKIELEZA KUWA WAMEJIPANGA KUKABILIANA NA
WAHAMIAJI HARAMU AMBAO WANACHANGIA ONGEZEKO LA UHALIFU NA UINGIAJI WA SILAHA
HARAMU NCHINI………
.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA LUTEN KANAL MSTAAFU ISSA MACHIBYA
AKITOA CHETI KWA MMOJA WA WANANCHI WALIOKABILIANA NA MAJAMBAZI NA KUWASHINDA
AKIELEZEA TUKIO LILILOSABABISHA WANANCHI HAO, KUTAMBULIWA NA
KUPEWA ZAWADI , KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIGOMA, FRAISSER KASHAI AMESEMA
WANANCHI HAO WALIKABILIANA NA MAJAMBAZI WAWILI WALIOKUWA NA MABOMU NA BUNDUKI
NAKUFANIKIWA KUMUUA MMOJA NA KUMYANG’ANYA BUNDUKI AINA YA SMG NA RISASI 160 KATIKA
TUKIO HILO AMBALO WATU KUMI WALITEKWA HUKU MMOJA WA WANANCHI HAO GEOFRE KWIGIZE
AKIELEZA KUWA MWENZAO MMOJA ALIPIGWA
RISASI MGUUNI NA WATATU WALIJERUHIWA KWA BOMU…
PICHA NA HABARI NA DEOGRATIUS NSOKOLO-KIGOMA
PICHA NA HABARI NA DEOGRATIUS NSOKOLO-KIGOMA
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.