NA EDWIN MOSHIAbiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la kampuni ya Ukinga maarufu kama Japanese lililokuwa likitoka mkoani Mbeya kwenda Ikonda Makete wameonja adha ya safari yao kwa mshituko mkubwa mara baada ya askari wa usalama barabarani waliokuwa njia panda ya Matamba kufyatua risasi hewani muda mchache baada ya kulisimamisha basi hiloTukio hilo la aina yake limetokea baada ya askari kutoka kituo kidogo cha polisi Matamba wilayani Makete mkoani Njombe kulisimamisha basi hilo kama ilivyo kawaida ili kufanya ukaguzi ambapo baada ya ukaguzi ilionekana basi hilo lenye namba za usajili T 446 CHG limebeba abiria kupita kiasiKufuatia hali hiyo, askari alilazimika kuzuia basi hilo kuendelea na safari huku akitaka abiria waliozidi kushuka na kutafutiwa usafiri mwingine pamoja na wahusika wa basi hilo(dereva na kondakta) kulazimika kulipa faini kutokana na kosa la kuzidisha abiria walilolifanya, ambapo kuliibuka malumbano kati ya dereva na askari hao wa usalama barabarani
Akijitetea mbele ya askari kuhusu kosa la kuzidisha abiria alilolifanya dereva huyo ambaye jina lake mwandishi wetu hakufanikiwa kulipata kutokana na hali halisi iliyokuwa eneo hilo, alimsikia dereva huyo akikiri kupakia abiria zaidi ya kiwango lakini akisema miongoni mwa abiria hao waliozidi ni wagonjwa pamoja na wengine walikuwa wanawahi msibani“afande kutokana na hali hiyo tunatambua kweli tumekosea abiria tumewajaza na kama unavyojua mazingira ya huku Makete abiria ni wengi lakini magari ni machache na kama tusingewabeba ni ngumu kwao kufika Ikonda hospitali kwa matibabu kwa kuwa gari ni hili moja tu” alisemaMaelezo hayo hayakufua dafu mbele ya askari na badala yake aliwataka kulipa faini ya kosa hilo ili iwe fundisho kwa wengine hali iliyowalazimu abiria waliokuwa kwenye basi hilo kushuka chini kujua kulikoni huku wakiwataka askari kuwaruhusu kuendelea na safari, na ndipo askari hao walipofyatua risasi hewani kama njia mojawapo ya wao kujihami kutokana na wingi wa abiria hao
Akizungumza na ripota wetu mmoja wa abiria aitwaye Ester kutoka Tukuyu aliyekuwa akielekea Ikonda hospitali kwa matibabu amesema wao kama abiria walimfuata askari na kumwambia kuwa wanaomba wawahishwe kutibiwa wao wachukue namba za gari waje kuwaadhibu baadaye lakini alishangazwa na askari kuanza kufyatua risasi hewaniMkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi anaruhusiwa kufyatua risasi pale anapoona maisha yake yapo hatarini kama njia mojawapo ya kujinasua na hatari iliyopo mbele yakeAmesema kilichosababisha mtafaruku huo ni kitendo cha askari huyo kumtoza faini ya shilingi 30,000/= dereva na kondakta wa basi hilo, ambapo kondakta alidai kuwa hana hela jambo ambalo halikuwaingia kichwani askari hao, na kugoma kuliruhusu gari hilo hadi pale watakapolipa faini ya kosa la kuzidisha abiria“Katika hali ya kawaida si rahisi kondakta kusafiri na gari tena la abiria bila kuwa na hela, hivyo kutokana na kukaa muda usiozidi dakika 15 wa mabishano abiria waliposhuka na kutaka kumfuata askari Yule mwenye silaha, aliwakataza abiria wasimfuate lakini alipoona wanazidi kumfuata, aliamua kufyatua risasi hewani kama njia ya kuwatawanya, na baadaye kondakta alilipa faini hiyo na gari likaruhusiwa kuondoka” alisema SP Kaiza
Jumatano, 29 Mei 2013
Related Posts
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni