RPC-NJOMBE
NA EDWIN MOSHI, MAKETE
Wakazi wa Makete mjini hasa waliokaribu na kituo cha polisi
Makete wamekumbwa na taharuki na mshituko wa hapa na pale kufuatia milio ya
mabomu iliyokuwa ikisikika tokea kituoni hapo
Hali hiyo iliyotokea leo hii imewashangaza wengi na kuwaacha
na sintofahamu huku wengi wao wakidhani kuwa yale ya liyotokea Arusha yamebisha
hodi Makete
Kutokana na taharuki hiyo, mtandao huu ulibisha hodi kituoni
hapo na kukutana na Mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza (Pichani)ambaye
alilitolea ufafanuzi suala hilo na kusema kwamba hali hiyo imetokea kwa kuwa
walikuwa wakifanya mazoezi ya kutuliza ghasia ama vurugu, ambapo iliwalazimu
kulipua mabomu
“Huo ni utaratibu wa jeshi kutokana na kufanya mazoezi
mbalimbali, mara ya mwisho tulilipua mabomu mwaka 2010 mwezi januari, tumekuwa
tukiwa katika mazoezi tunafanya hivyo na hii pia inasaidia kuweka askari wetu
tayari, na pia wananchi kufahamu kama hali hiyo ikitokea hali inakuwaje”
alisema Kaiza
Akizungumzia kuhusu kutoa taarifa kwa wananchi, SP Kaiza
amesema wangeweza kutoa taarifa kwa wananchi ingawa walitoa taarifa kwa uongozi
wa wilaya, lakini wakati mwingine mabomu hulipuka eneo lolote bila taarifa na
kwa kufanya hivyo kunasaidia kuwaweka tayari wananchi
Amesema mabomu hayo hayana madhara na hakuna tukio baya
lililotokea, hivyo kuwataka wananchi kuondoa hofu na kuendelea na shughuli zao
kama kawaida
0 comments:
Chapisha Maoni