Meneja
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa akimsikiliza jambo na
Mkurugenzi wa Timu ya Dunia wa wa kampuni inayohusika na uuzaji wa dawa
asilia zenye ubora wa kimataifa ya GNLD Tanzania, Bi.Grace Rubambey,mara
baada ya hafla ya kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kuanza kulipia
bidhaa mbalimbali zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma ya M-Pesa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria halfa hiyo ya kuwawezesha
wateja wa kampuni ya GNLD kuanza kulipia bidhaa mbalimbali zenye ubora
wa kimataifa kupitia huduma ya M-Pesa.
Mmoja
wa wateja wa kampuni inayouza bidhaa za asilia pamoja na dawa zenye
ubora wa kimataifa (GNLD)akiuliza swali juu ya ulipaji pesa kupitia
huduma ya M-PESA,wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa (kushoto)
akionyesha njia muhimu za M-PESA pindi mteja akiwa analipia Ankara zake
akiwa amenunua bidhaa na dawa asilia zenye ubora wa kimataifa za GNLD
Tanzania,wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuwawezesha wateja wa kampuni
hiyo kuanza kulipia bidhaa mbalimbali zenye ubora wa kimataifa kupitia
huduma hiyo,wanaoshuhudia katikati Mwakilishi wa GNLD Tanzania, Daniel
Mutiso,Rais wa vikundi wa GNLD Tanzania, Bi. Dora Juma.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa (kushoto) pamoja
na Mwakilishi wa GNLD Tanzania, Daniel Mutiso, wakipongezana mara baada
ya kukamilisha makubaliano ya kibiashara na kampuni inayohusika na
uuzaji wa dawa asilia zenye ubora wa kimataifa ya GNLD Tanzania,ambayo
itawawezesha wateja wa kampuni hiyo kulipia Ankara zao kupitia huduma
ya M-PESA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wateja GNLD sasa kulipia bidhaa kwa njia ya
M-Pesa Dar es Salaam, Mei 6, 2013 ... WATEJA wa huduma ya M-Pesa nchini
sasa watanufaika na huduma hiyo ya teknolojia ya simu kwa kuwawezesha
watanzania kwa mara ya kwanza kulipia bidhaa za kampuni ya GNLD Tanzania
inayouza dawa asilia zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma hiyo ya
M-Pesa.
Huduma ya M-Pesa, imeendelea kurahisisha maisha ya
watanzania kwa kupanua huduma zake katika sekta mbalimbali za kibenki
wakati huu ikishuhudia kuingia katika ushirikiano kati ya Kampuni ya
Vodacom Tanzania na Kampuni inayohusika na uuzaji wa dawa asilia zenye
ubora wa kimataifa ya GNLD Tanzania.
Mpango huu umelenga kunufaisha wateja kwa kuweza kulipia bidhaa za GNLD kwa njia ya huduma hiyo ya M-Pesa.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rukia
Mtingwa, wateja ambao wako tayari kulipa kwa ajili ya bidhaa za GNLD
hawana sababu tena ya kubeba fedha kwa sababu za usalama.
"M-Pesa ni
huduma ambayo ni salama na ya haraka. Kutokana na ushirikiano huu,
wateja hawatakuwa na sababu ya kupoteza muda wao kwenda kwa wakala wa
GNLD kulipa kwa ajili ya bidhaa fulani. Wanachotakiwa kufanya ni kutumia
huduma ya Vodacom M-Pesa na kufanya malipo," anasema Mtingwa.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa GNLD Tanzania, Daniel Mutiso, anasema kwamba
GNLD itaendelea kuhakikisha kwamba inaendelea kutoa huduma yenye kiwango
cha juu cha ubora ili kukuza afya bora kwa kila mtu.
"Ushirikiano
huu ni wa kwanza na wa aina yake katika soko hili. Hivyo tunajisikia
furaha kufanya uzinduzi huu leo kwasababu utaweza kusaidia kila mtu
katika nchi hii," anasema Mutiso.
Kulipia bidhaa za GNLD kupitia
huduma ya M-Pesa, wateja watakiwa kupiga *150*00# na kuchagua Malipo na
kisha kuingiza namba ya Biashara ambayo ni 000221na kufuatiwa na namba
ya akaunti ikifuatiwa na Kiasi kisha Namba ya Siri (PIN) na mwisho
kufanya uthibitisho.
0 comments:
Chapisha Maoni