Wafanyakazi
wa mkoa wa Singida na wananchi kwa ujumla, waungana na wenzao
kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani (mei mosi) yaliyofanyika jana kimkoa
kwenye uwanja wa michezo wa Namfua.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,akipokea maandamano ya wafanyakazi jana
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi dunia
zilizofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,jana akihutubia baadhi ya wafanyakazi na
wananchi wa mkoa wa Singida waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku
ya wafanyakazi duniani (mei mosi) zilizofanyika kwenye uwanja wa
Namfua.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,jana akimkabidhi mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Fortunata Mallya cheti cha mfanyakazi
bora baada ya mkurugenzi huyo kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa
halmashauri ya Manyoni kwa mwaka wa 2013/2014.
Baadhi
ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa mkoa wa Singida,waliohudhuria
sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (mei mosi)
zilizofanyika jana kimkoa katika uwanja wa Namfua mjini Singida.
Kikundi
cha uhamasishaji cha kata ya Kindani manispaa ya Singida kikitoa
burudani kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani zilizofanyika
kimkoa kwenye uwanja wa namfua mjini Singida.
Baadhi
ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali mkoani Singida,waliohudhuria
maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi duniani zilizofanyika kimkoa
katika uwanja wa namfua mjini Singida.
(Picha zote na Nathaniel Limu).
0 comments:
Chapisha Maoni