Pichani Professor Jay akiwa na
Kiboya,mdau mkubwa wa muziki nchini ambaye pia ni mwanachama wa CHADEMA.
Picha kwa hisani ya Twitter ya Professor.
Habari ambazo zinatambaa hivi sasa mtandaoni ni kwamba msanii maarufu
na miongoni mwa wanaoaminika kuwa waasisi wa muziki wa Hip Hop nchini
Tanzania, Professor Jay (jina halisi Joseph Haule), amejiunga rasmi na harakati za siasa nchini kwa kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Professor Jay ambaye tungo zake mara kwa mara zimekuwa zikijikita
katika kutetea maslahi ya wananchi, amejiunga na CHADEMA huko Dodoma
ambapo amekabidhiwa rasmi kadi ya uanachama.
Zoezi hilo limesimamiwa na John Mnyika, Mbunge wa Ubungo na Joseph
Mbilinyi (Sugu) Mbunge wa Mbeya Mjini na kushuhudiwa na wanachama
wengine kadhaa ambao aidha ni wanamuziki pia au wadau wa karibu wa
muziki.
Bila shaka kujiunga kwa Professor Jay na CHADEMA kunaashiria kwamba
yupo mbioni kugombea Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Professor Jay ni mwenyeji wa Mikumi-Morogoro na hivyo haitoshangaza kama
ataamua kugombea katika jimbo hilo hapo mwaka 2015.
Professor Jay akikabidhiwa kadi na Mh.Joseph Mbilinyi.
0 comments:
Chapisha Maoni