Big Brother Africa ni Shindano la UHALISIA wa maisha, washiriki wa shindano hili wataonyeshwa moja kwa moja - wakiwania kiasi $300,000 USD, sawa Tsh 480milioni, huku vigezo na masharti vikitajwa kuwa ni washiriki wenye mvuto kwa akili na mwonekano, ndiyo watakaoingia katika jumba hilo.
MTANGAZAJI WA BIG BROTHER THE CHASE OSAKIODUWA IK
Mtangazaji maarufu "IK Osakioduwa" anarudi kwa mara nyingine kuendesha The Chase.
"Big Brother Africa ni shoo ya kipekee, kila msimu una muda maalumu na ladha yenye msisimko, nimefurahi kuwa mwenyeji tena wa shindano hili, kama kawaida yangu nitaanza kuwapa changamoto washiriki siku kwanza tu! Watakapopita jukwaani mbele ya lango la Big Brother", alisema IK aliye mtangazaji maarufu wa televisheni na redio.
0 comments:
Chapisha Maoni