Mwenyekiti
wa shirika lisilo la kiserikali la SIAG la mjini Singida, Theresia
Mwakasasa akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya siku moja iliyohusu
madhara ya ukeketaji na manyanyaso kwa wanawake.Wa kwanza kulia ni
Agnete Strom afisa wa shirika la STORM la nchini Norway anayefuata ni
Chiku Alli, afisa wa afya na masuala ya jamii katika serikali ya
Norway.Wa pili kushoto ni mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la
Fokus la nchini Norway, Anton Popic.
Mratibu
wa shirika lisilo la kiserikali la SIAG la mjini Singida, Hadija Juma
akitoa mada yake ya utekelezaji wa shughuli ya mapambano dhidi ya
vitendo vya ukeketaji.
Afisa
wa afya na masuala ya jamii katika serikali ya Norway, Chiku Alli
akitoa mada yake iliyohusu elimu juu ya madhara yatokanayo na vitendo
vya ukeketaji.
Afisa
wa afya na masuala ya kijamii wa serikali ya Norway,Chiku Alli
akichangia mada zilizokuwa zikitolewa zinazohusu madhara yatokanayo na
vitendo vya ukeketaji.
Baadhi
ya wanasemina ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji iliyofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hill mjini Singida.
Baadhi
ya wanasemina wakicheza muziki wakati wa mapumuziko ya semina ya
mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji.
(Picha zote na Nathaniel Limu).
0 comments:
Chapisha Maoni