Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.(Picha na Maktaba).
Na Johary Kachwamba-Maelezo
Ujenzi
wa Kivuko chenye uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilometa 40 kwa saa
moja, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi nane kwa lengo la kupunguza
msongamano wa magari jijini Dar-es-salaam.
Kivuko
hicho kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Bagamoyo na Kigamboni
kupitia Tegeta na vituo vigine sita (6), kina uwezo wa kubeba zaidi ya
abiria 300.
Akizungumza
jijini Dar-es-salaam wakati wa kusainiwa rasmi mkataba wa manunuzi ya
kivuko hicho, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amesema pesa zote
zilizotumika katika manunuzi ya kivuko hicho zimetolewa na Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) na hivyo ni pesa za wananchi.
“kupanda
kwa nauli ya vivuko vyetu na usimamizi mzuri wa pesa zinazopatikana
katika vivuko hivyo ndiyo matunda ya kupatikana kwa kivuko hiki, hakuna
pesa ya msaada hapo ni pesa za watanzania” alisema Waziri Magufuli.
Mradi
huu wa serikali umeanza na jiji la Dar-es-salaam na kuahidi kufanya
hivyo hata kwa mikoa mingine inayoweza kutumia aina hii ya usafiri, kama
Kigoma na Mwanza.
Aidha
Serikali ameiasa kampuni yenye dhamana ya kujenga kivuko hicho kufuata
makubaliano yaliyowekwa, kwa kukamilisha kazi hiyo kwa kiwango na wakati
ili Watanzania wapate mbadala mwingine wa usafiri haraka.
kampuni
ya M/S Johns Gram Hanssen kutoka nchini Denmark ndiyo iliyoshinda
Zabuni ya ujenzi wa kivuko baada ya kuzishida kwa vigezo kampuni zingine
11 kutoka nchi mbalimbali, na gharama ya manunuzi ni dola za kimarekani
dola 4,980,000/= sawa na Bilioni 7.91 shilingi za Tanzania.
Mwezi
julai, 2012 TEMESA iliitisha mkutano wa Wadau kujadili jinsi ya kuweza
kupunguza na kisha kumaliza kabisa msongamano wa magari jijini
Dar-es-salaam, miongoni mwa wadau ni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA).
Moja
ya mapendekezo ilikuwa ni ujenzi wa kivuko cha abiria kitakachotoa
huduma kati ya Kigamboni na Bagamoyo, nasasa ununuzi wa kivuko hicho
umekamilika, kwa usimamizi wa TAMESA ikushirikiana kwa karibu na Wizara
ya Ujenzi.
Mwenyekiti
wa bodi ya ushauri TEMESA, Prof. Idrissa Mshoro amesema SUMATRA na TPA
watawajibika kukagua Ubora wa kivuko mara kitakapo kamilika katika
karakana ya West Marine, nchini Bagladesh, kwakuwa ujenzi wa kivuko hiki
unafanyika nchini humo.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Johnny Flentø, amedhibitisha ubora wa
huduma za kampuni yenye dhamana ya M/S Johns Gram Hanssen, huku
akiridhia ujenzi kufanyikia Bangladesh kwakuwa watajenga haraka na kwa
bei nafuu.
0 comments:
Chapisha Maoni