Waziri mkuu wa Uingereza
bwana David Cameron amesema kitendo kilichofanywa na mshambuliaji wa Liverpool
Luis Suarez kumng’ata bila huruma Branislav Ivanovich kimekua ni mfano mbaya
sana katika soka la nchi hiyo..
"kama baba na binadamu wengine nafikiri
tunapaswa kuweka adhabu kali sana wenye tabia kama hizi" alisema bwana
Cameron.
Hata hivyo Kocha wa Liverpool Brendan
Rodgers amelalamikia kauli ya kwanza aliyoitoa waziri mkuu huyo kwamba
ilichangia kwa kiasi kikubwa mchezaji wake kupewa hukumu kubwa ya kufungiwa
mechi kumi.
Kabla ya kamati kukaa ili kujadili
adhabu hiyo bwana Cameron alikaririwa akisema kwamba ”itakua ni kitu
kisichoeleweka endapo tu kamati hiyo itachukulia kwamba wachezaji maarufu siku
zote ni watu wa kuigwa”kauli ambayo iliwafadhaisha na kuwastua Liverpool.
"Hii ni mara yangu ya kwanza
kusikia kamati iliyo huru kuingiliwa na watu wengi na viongozi wa juu wa
nchi..alisema Rogers."
Hata hivyo bwana Cameron alijibu
mapigo ijumaa hii asubuhi na kumbwatukia bwana Rogers kwamba yeye yupo huru
kutoa maoni yake pasipo kujali cheo chake.
"mimi nimeweka mawazo yangu
sawa …mimi kama baba niliyekua nikiangalia mchezo ule bwana Cameron …mimi nina
mtoto mwenye umri wa miaka saba ambaye ni mpenzi mkubwa wa mchezo wa mpira wa
miguu,kwahiyo wakati wachezaji wanapokuwa na tabia kama hizi ni mfano mbaya
sana kwa kizazi cha vijana wadogo wa taifa letu….alimalizia bwana Cameron
0 comments:
Chapisha Maoni