Searching...
Jumanne, 16 Aprili 2013

MSIBA MZITO CHUO KIKUU TUMAINI-DAR ES SALAAM

CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA DAR ES SALAAM KIMEKUMBWA NA MSIBA MZITO BAADA YA MWANAFUNZI WA CHUO HICHO ALIYEKUA AKISOMA KITIVYO CHA SAYANSI YA JAMII GILBERT MELIARA KUFARIKI DUNIA SIKU CHACHE ZILIZOPITA KUTOKANA NA UGONJWA WA TYPHOD.
VILIO VILIRINDIMA WAKATI WAHADHIRI,WAFANYAKAZI,WANACHUO,WAZAZI,NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALIPOKUTANA KATIKA UKUMBI WA CHUO HICHO CAMPUS YA MWENGE BARABARA YA COCACOLA KUMUAGA MAREHEMU TAYARI KUSAFIRISHWA KWENDA ARUSHA KWA MAZISHI.
AKIZUNGUMZA KATIKA IBADA YA KUMUAGA MAREHEMU GILBERTH BABA MDOGO WA MAREHEMU ALISEMA MAREHEMU ALIKUA NDIYE TEGEMEO KUBWA NA NGUZO YA FAMILIA YAKE KAULI AMBAYO ILIAMSHA VILIO VIKUBWA NDANI NA NJE YA UKUMBI HUO
ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA KUMUAGA BWANA GILBERT MELIARA

 WANACHUO WAKIWA KATIKA MAKUNDI MAKUNDI WAKISUBIRI MWILI WA MPENDWA WAO GILBERT KUWASILI CHUONI HAPO TAYARI KUMUAGA.


 MWILI WA MAREHEMU UKAWASILI NA HAPO NDIO UNAINGIZWA UKUMBINI TAYARI KWA IBADA YA KUMUAGA
 MWILI WA MAREHEMU UKIWA NDANI YA UKUMBI TAYARI KWA IBADA YA KUMUAGA NA PICHA YAKE IKIWA JUU YA JENEZA
 MCHUNGAJI AKIONGOZA IBADA YA KUMUAGA MAREHEMU GILBERT MELIARA.
 MWANDISHI WA HABARI MKONGWE NA MZOEFU JERRY MURO AKICHUKUA HABARI.
 UTULIVU ULITAWALA WAKATI WA MAOMBEZI YA KUMUAGA GILBERT MELIARA KATIKA UKUMBI WA CHUO KIKUU TUMAINI KAMPASI YA DAR ES SALAAM
 WALIOJITOKEZA KUMUAGA GILBERT WAKIWA WANAMSIKILIZA MCHUNGAJI KWA MAKINI
  BABA MDOGO WA MAREHEMU AKISOMA HISTORIA YA MAREHEMU
 RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUONI HAPO BWANA ABDULRAHAMAN BWAYU AKITOA NENO LA KUMUAGA MAREHEMU KWA NIABA YA WANACHUO

 WANACHUO WAKIMUAGA MWENZAO HUKU WENGINE WAKILIA KWA HUZUNI NA HISIA HADI KUZIMIA.





 CHUO KILIGUBIKWA NA MAJONZI NA HUZUNI KUBWA

HATIMAYE SAFARI YA KUMPELEKA GILBERT NYUMBANI KWAO ARUSHA KWAAJILI KUHIFADHIWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE NDIO HAPO IKAWADIA
MWILI WA MAREHEMU UKAONDOKA HUKU NYUMA WANACHUO WAKABAKI NA MAJONZI NA HUZUNI PASIPO KUAMINI KAMA KWELI GILBERT MELIARA HAWATAMUONA TENA.
BWANA AMETOA,AMETWAA JINA LA BWANA NA LIHIMIDIWE AMINA.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!