Searching...
Jumatatu, 15 Aprili 2013

KAMPUNI YA OLAM YATOA MSAADA MBEYA

KAMPUNI ya Olam Tanzania limited inayojishughulisha na ununuzi wa zao la kakao wilayani Kyela mkoani Mbeya imetoa msaada wa mifuko 20 ya saruji yenye thamani ya Tsh,350000,  katika shule ya msingi Mbogera iliyopo kata ya Kyela kati kwa lengo la kusaidia sekta ya elimu wilayani hapa,
 Akizungumza  na ripota wetu wakati wa zoezi hilo meneja wa kampuni hiyo Godfrey Okungu alisema kuwa kampuni yake imetoa msaada huo ili kuendeleza ujenzi wa madarasa unaoendelea shuleni hapo na kwamba wataendelea kusaidia ili kukamilisha ujenzi huo,
 Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Godfrey Sanga ameipongeza kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa elimu na kuamua kutoa msaada huo utakaoongeza kasi ya ujenzi ambapo wananchi wanachangia nguvu kazi na kujenga hadi kwenye mtambao wa panya na serikali watapaua majengo hayo kama utaratibu ulivyopangwa,
 Sanga alisema kuwa kupokea  mifuko hiyo ya saruji utawapelekea wao kukamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa kwa kuwa shule hiyo inamadarasa manne tu huku zoezi la kufundisha  likiwa gumu,na kuwa ujenzi huo utakamilika mwezi wa 11 mwaka huu ambao utandoa msongamano wa wanafunzi madarasani,
 Mkuu wa shule hiyo  Mwl,Ally Mwangosi alisema kuwa kupokea msaada huo kutawapa msukumo wanafunzi huku wakijua kuwa ujenzi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakaoondoa changamoto ya upungufu wa madarasa uliodumu kwa muda mrefu shuleni hapo,
 Mwl Mwangosi aliongeza kuwa shule hiyo inakabiliwa na upugufu  wa madarasa 11 yaliyopo ni ma nne huku matundu ya vyoo yanayohitajika ni 36 yaliyopo ni 20 hivyo wanahitaji nguvu ya wadau mbalimbali katika kuchangia na kukamilisha ujenzi huo ili wanafuzi wasome kwa amani na kuwaelewa waalimu na kufanya vizuri pindi wanapohitimu darasa la saba,
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha mbogera Shabani Lusekelo alisema kuwa mbali na kuipongeza kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo,pia atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha sementi hizo zinatumika ipasavyo bila kuwepo na ufisadi ili kujenga imani na  wadau hao ili waendelee kutoa  misaada katika shule hiyo,
 Mkuu wa wilaya  ya Kyela aliyewakilishwa na afisa Tarafa ya Ntebela Rafael Kilale kwa upande wake aliipogeza kampuni hiyo kwa kusaidia ujenzi  shuleni hapo na kwamba majengo hayo yatakapofikia mtambao wa panya serikali kupitia Halmashauri ya wilaya itayapaua majengo hayo yatakayoongeza tija kwa wanafunzi shuleni hapo
 Na Edwin Moshi

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!