ENEO LA NIGER DELTA.
Maafisa wa usalama nchini Nigeria wamepata miili 11
ya wanajeshi 12 waliouawa katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la
Niger Delta siku ya Ijumaa.
Polisi wanasema kuwa baadhi ya miili hiyo ilikuwa imekatwakatwa na kuchomwa kiasi cha kutotambulika.Hata hivyo, watu wengi ni masikini na hivyo huchukizwa na serikali pamoja na makampuni ya mafuta kwa kutowafaidisha na rasilimali hiyo.
Mwishoni mwa wiki, kundi la wapiganaji wa MEND, walisema kuwa walivamia mashua iliyokuwa imewabeba polisi katika jimbo la Bayelsa na kuwaua polisi.
Msemaji wa polisi, Alex Akhigbe alisema kuwa miili 11 ilipatikana wakati polisi mmoja hadi hivi sasa hajulikani aliko.
Miili hiyo ilisafirishwa kwa boti hadi katika eneo la Yenagoa ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo kuchukuliwa na familia zao.
Aidha mwishoni mwa wiki polisi walikana kuwa mauaji hayo yanaweza kuhusishwa na kufungwa kwa Henry Okah.
Badala yake walisema kuwa yalihusu mgogoro wa malipo ya mishahara ya wapiganji hao waliokuwa wanalipwa baada ya kukomesha harakati zao za mapigano dhidi ya serikali.
Mashua za polisi waliokuwa wanamsindikiza mwenzao kwa mazishi, zilikumbwa na hitilafu na hivyo kulengwa na wapiganaji hao kwa mashambulizi.
Kundi la Mend lilikuwa linafanya vurugu kutaka kupewa sehemu ya rasilimali za mafuta Kusini mwa Nigeria lakini likasitisha harakati zao mwaka 2009, wakati waliposalimisha silaha na kusamehewa.
Habari na picha kwa hisani ya bbc-swahili .
0 comments:
Chapisha Maoni