Mtambo wa Korea Kusini wa kukinga mashambilizi ya makombora.
Korea Kusini imeimarisha hali yake ya tahadhari
kufuatia habari kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la
kombora lake moja la masafa ya kadiri.
Marekani na Korea Kusini zinasema kuwa hadi
kufikia sasa wanazo habari kwamba mojawapo ya kombora lililo na uwezo wa
kushambulia umbali wa kilomita 3,000 ambalo halijafanyiwa jaribio
limejazwa mafuta tayari kulipuliwa.Pyongyang imekuwa ikitoa vitisho dhidi ya kambi za kijeshi za Korea Kusini, Japan na Marekani.
Vitisho hivyo vinakuja baada ya vikwazo vipya na vikali zaidi kutolewa dhidi ya Korea Kaskazini mwezi jana kufuatia
jaribio lake la tatu la kinyuklia.
Mbali na hayo, uchunguzi wa hapo awali uliofanywa na Korea Kusini kuhusu uvamizi wa mtandao, mwezi jana na ambao uliathiri idadi kubwa ya benki na mitambo ya kupeperusha matangazo umeonyesha kuwa wa kulaumiwa kwa hilo ni Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini inaaminika kukamilisha mipango yake ya kuzindua kombora baada ya kuhamisha makombora yake mawili upande wa Pwani mwa nchi.
Ili kujibu tishio hilo, Korea Kusini kwa ushirikiano na Marekani zimeimarisha mitambo yake ya kuchunguza shambulio lolote.
Korea Kaskazini ilizindua Kombora lake wakati wa gwaride la jeshi mwaka 2010 lakini bado haijalifanyia jaribio lolote.
Jaribio hilo linaweza kufanyika wakati wowote kuanzia sasa , kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo
Yun Byung.
Habari kwa hisani ya BBC- Swahili.
0 comments:
Chapisha Maoni