MANDELA ATOKA HOSPITALI.
Rais mstaafu wa Afrika Kusini,Bwana Nelson
Mandela, ameruhusiwa kutoka hospitalini ambako alikua akitibiwa homa ya mapafu
yaani pneumonia kwa siku kumi.
Serikali imetoa taarifa kusema kuwa
hali ya Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, imetengemaa sana na ataendelea
kutibiwa nyumbani.
Hali ya Bwana Mandela ilishtusha
mwezi Disemba mwaka jana ambapo alilazwa hospitalini kwa karibu majuma matatu kwa
sababu ya ugonjwa wa mapafu na kijiwe kwenye nyongo.
Rais Zuma aliwashukuru matabibu na
wauguzi kwa jitihada yao ya kumuungalia Bwana Mandela kwa uzuri.
Habari na BBC – Swahili.
0 comments:
Chapisha Maoni