Bayern Munich, wameshinda taji lao
la 23 la Ligi ya soka Ujerumani – Bundesliga na kuweka rekodi ya kuwa washindi
wa mapema kabisa wa Ligi kuwahi kushuhudiwa Ujerumani zikiwa zimesalia mechi
sita msimu kukamilika
Sasa Bayern wamesalia na mechi sita
wakiandaa gwaride la kulionyesha taji la Bundesliga, baada ya kiungo Bastian
Schweinsteiger kufunga bao la kiustadi kwa njia ya kisigino na kuwapa ushindi
wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Eintracht Frankfurt.
Vijana hao wa Mkufunzi Jupp Heynckes
wamemaliza uongozi wa miaka miwili wa Borussia Dortmund kwa kushinda taji la 22
la Bundesliga mapema kuliko klabu nyingine yoyote katika historia ya miaka 50
ya ligi hiyo. Bayern walikosa nafasi baada ya Xherdan Shaqiri kuupiga mlingoti
wa goli, wakati David Alaba akikosa kufunga mkwaju wa penalti. Ushindi huo
uliwapa Bayern uongozi wa jumla ya pointi 75
Jupp Heynckes amesema ni vizuri sana
kushinda tena taji baada ya miaka 23. aliwaongoza Bayern kutwa mataji ya mwaka
wa 1989 na 1990 wakati akiwa kocha. Heynckes atampisha Mhispania Pep Guardiola
mwishoni mwa msimu huu wakati ambapo Bayern huenda watakuwa wameongeza mataji
mengine mawili, Champions League na Kombe la Shirikisho. Nahodha wa Bayern
Philip Lahm anasema sasa wameangazia macho yao katika mchuwano wa marudio wa
robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.
picha na habari kwa hisani ya DW-Swahili.
picha na habari kwa hisani ya DW-Swahili.
0 comments:
Chapisha Maoni