Searching...
Jumapili, 21 Aprili 2013

LEO NDIO LEO ENGLAND LIVERPOOL KUMVAA BENITEZ (LIVERPOOL Vs CHELSEA) WAMTABIRIA MEMA NA MABAYA,SOMA HAPA UONE

 JUU BENITEZ AKIWA NA JESI YA CHELSEA NA CHINI AKIWA NA SCUF YA LIVERPOOL NA WACHEZAJI WA LIVERPOOL.

LEO NDIO LEO HUKO NCHINI ENGLAND KWA WALE WAPENZI WA SOKA WATASHUHUDIA MOJA YA MECHI NGUMU KATIKA LIGI HIYO PALE MATAJIRI WA LONDON VIJANA WA TAJIRI WA KIRUSI ALIYEBOBEA ROMAN ABRAMOVICH WATAKAPOSAFIRI HADI JIJINI LIVERPOOL KUWAKABILI MAJOGOO WA ANFIELD LIVERPOOL KATIKA MECHI AMBAYO ITAKUA NA MSISIMKO WA KIPEKEE KWANI KWA MARA YA KWANZA ALIYEKUA KOCHA WA LIVERPOOL ATAKUA AKISHUKA KATIKA UWANJA HUO AKIWA NA TIMU PINZANI YAANI CHELSEA THE BLUES.
WACHAMBUZI WA SOKA WANATABIRI KWAMBA LEO NDIO UNAWEZA UKAWA MWISHO WA BENITEZ KUIONGOZA CHELSEA KULINGANA NA MATOKEO ATAKAYOYAVUNA LEO UGENINI KWA LIVERPOOL TIMU YAKE YA ZAMANI AMBAYO WENGI WANADAI BADO ANAYO MAPENZI YA DHATI KWA KLABU HIYO.
WENGI PIA WAMETABIRI KWAMBA ANAWEZA AKAZOMEWA SANA NA MASHABIKI WA LIVERPOOL HUKU WENGINE WAKITABIRI KWAMBA ATAPOKELEWA KAMA SHUJAA WA LIVERPOOL KAMA VILE AMBAVYO ALIVYOPOKELEWA CHRISTIAN RONALDO ALIPOREJEA KATIKA UWANJA WAKE WA ZAMANI NGOME KONGWE OT AKIWA NA KLABU YA MADRID WIKI CHACHE ZILIZOPITA.
CHELSEA KATIKA MSIMAMO WA LIGI NI YA NNE IKIWA NA ALAMA 61 IKIWA IMESHACHEZA MICHEZO 32 WAKATI LIVERPOOL INAKAMATA NAMBA SABA IKIWA NA ALAMA 50 HUKU IKIWA IMESHUKA DIMBANI MARA 33 MCHEZO MMOJA MBELE YA CHELSEA.
LEO CHELSEA ITABIDI IPIGANE KUFA AU KUPONA ISHINDE ILI IWEZE KUWA NA MATUMAINI YA KUWEPO KWENYE TIMU NNE ZA JUU VINGINEVYO ITAKUA HATARI SIKU WATAKAPOKUTANA NA TOTTENHAM KATIKA MCHEZO WA KIPORO KWANI TIMU HIZO ZOTE ZINA NAFASI YA KUSHIKA NAMBA TATU AU NNE KATIKA MSIMAMO WA LIGI HIYO NAFAZI AMBAZO ZITAWAWEZESHA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA MASHINDANO MAKUBWA,YENYE FEDHA,USHINDANI,HESHIMA NA MSISIMKO MKUBWA DUNIANI 
KIPI KITAKUA VIPI,UTABIRI UPI UTAKUA WA KWELI,NANI ATAIBUKA MSHINDI TUSUBIRI TUONE HAPO JIONI YA LEO.
MECHI HII ITAPIGWA MAJIRA YA SAA KUMI NA MOJA KAMILI JIONI KWA SAA ZA TANZANIA,NA ILE YA TOTTENHAM NA MANCHESTER CITY ITAPIGWA SAA NANE NA NUSU MCHANA.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!