Searching...
Alhamisi, 18 Aprili 2013

ZIARA YA CCM KILOSA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana afungua  Shina  la wajasiriamali, wakereketwa wa CCM la Dinima, Kilosa, prili 17, 2013, akia katika ziara kukagua na kuimarisha uhai wa Chama mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa CCM shila namba 15, tawi la CCM Mbuni B, Kilosa, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani mkoani Morogoro, Aprili 17, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 17, 2013, kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Umoja mjini Kilosa mkoani Morogoro.
  Katibu wa NEC, Itrikadi na Uenezi, Nape Nnauye (Kushoto), akiwa na wanachama wa shina namba 15, tawi la CCM, Mbuni B, Kilosa, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) alitembelea shina hilo na kuzungumza na wanachama hao akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM, Aprili 17, 2013.
Viongozi kuanzia ngazi za mashina wa CCM katika wilaya ya Kilosa, wakizungumza na Kinana kwenye ukumbi wa Comfort, wilayani humo mkoani Morogoro, Aprili 17, 2013
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni kwenye Shina  la wajasiriamali wakereketwa wa CCM la  Dinima, Kilosa, mkoani Morogoro, alipofika kwenye shina hilo akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 17, 2013.
KILIMO KWANZA:
 Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Sif Khatib akitazama mahidi yalivyostawi kwenye shamba la mkulima maarufu wa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.Picha na Bashir Nkromo

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!