NYUMBA MBILI NA OFISI MBILI ZIMECHOMWA MOTO JIONI HII HUKO LIWALE MKOANI LINDI BAADA YA WAKULIMA WA KOROSHO KUSHINDWA KUZUIA JAZBA WALIYOKUA NAYO KUFUATIA KUPUNGUZIWA MALIPO YAO KUTOKA SHILINGI MIA SITA KWA KILI MOJA YA KOROSHO HADI SHILINGI MIA MBILI.
AKIZUNGUMZA NA BLOG HII USIKU HUU KUTOKA LIWALE MWANAHABARI WETU AMESEMA NYUMBA ZILIZOCHOMWA MOTO NI PAMOJA NA NYUMBA YA MBUNGE WA LIWALE MHESHIMIWA SEIF MOHAMED MITAMBO NA OFISI YAKE PAMOJA NA NYUMBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MSINGI LIWALE B PAMOJA NA OFISI YAKE.
HABARI ZAIDI ZINASEMA MKE WA MENEJA WA CHAMA CHA MSINGI ILULU AMELAZWA HOSIPTALINI KUFUATIA MSTUKO ALIOUPATA BAADA YA WATU HAO KUVAMIA NYUMBA YAKE NA KISHA KUICHOMA MOTO.
JESHI LA POLISI LILILAZIMIKA KUINGILIA KATI VURUGU HIZO KWA KUPIGA MABOMU YA MACHOZI ILI KUSAIDIA KUWATAWANYA WATU HAO ILI KUEPUSHA HASARA ZAIDI.
Jumanne, 23 Aprili 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

0 comments:
Chapisha Maoni