Zaidi ya watu 2,000 mashuhuri duniani wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Margaret Thatcher katika mkusanyiko mkubwa wa watu tangu mazishi ya mama yake malkia wa Uingereza mwaka 2002.
Polisi elfu nne walishika doria mjini London , mji ambao umejionea idadi kubwa ya watu waliojitokeza kushuhudia mazishi hayo.
Kulikuwa na taarifa za maandamano dhidi ya Thatcher ingawa sio makubwa kama ilivyotarajiwa.
Mkusanyiko wa watu katika kanisa la Mtakatifu Paul ulijumuisha familia ya Thatcher pamoja na waziri wakuu wa zamani akiwemo Tony Blair, Gordon Brown na Sir John Major, mawaziri wa sasa na wale waliohudumu kama serikali ya Bi Thatcher.
Majonzi yalishuhudiwa pamoja na kicheko mara kwa mara huku Askofu wa London, Richard Chartres akiwakumbusha watu kuhusu Thatcher na kumsifu kwa ukakamavu wake.
Thatcher alikuwa na ushawishi na mwenye utata na alifariki dunia wiki jana baada ya kuugua kiharusi
Maelfu ya watu na maofisa wa kijeshi walipiga foleni katika barabara kuu za mjini London kuusindikiza mwili wa Bi Thatcher.
Habari na BBC-Swahili
0 comments:
Chapisha Maoni