Katika hali ya kushangaza ni kwamba huenda timu ya QPR ambayo imeshatangaza kumsajili mkongwe wa Manchester United Rio Ferdnad huenda uamuzi huo ukabatilishwa baada ya makubaliano ya mshahara wa Rio Ferdinand katika klabu hiyo ya QPR kuleta utata.
Rio Ferdinand wakati akiwa anakipiga na timu ya Manchester United alikua akilipwa kitita cha paundi laki mbili kwa wiki ambapo sasa anataka kulipwa sio chini ya moja ya tatu ya mshahara wake huo akiwa Man U ambapo ni paundi 67,000 ambazo QPR wanaona ni nyingi sana kulingana na malipo ya wachezaji wengine.
Kwa sasa Rio Ferdinand yupo na mkataba mfupi wa kuchambua mechi za kombe la dunia katika kituo cha BBC.

0 comments:
Chapisha Maoni