Mchezaji wa timu ya taifa ya Italia mtukutu Mario Balotelli ameweka wazi kwamba anataka kujiunga na Arsenal kutokana na kuchoshwa na shutuma za kila siku kila mtaa anaopita nchini Italia akishutumiwa kwamba alicheza chini ya kiwango kwa makusudi hadi timu yao ya taifa ikaondoshwa katika michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazili.

Baloteli akirejea nyumbani akiwa na mchumba wake baada ya kuondoshwa kunako kombe la dunia huko nchini Brazili.
Taarifa zinasema kwamba endapo kocha wa Arsenal Arsene Wenger ataendelea kusua sua kumsajili Baloteli huenda akajikuta akiambulia vumbi kutokana na juhudi anazozifanya Mourinho za chini chini za kumsajili Baloteli ili kuwa mchezaji mwenza wa Diego Costa katika safu ya ushambuliaji ya Chelsea msimu ujao.
0 comments:
Chapisha Maoni