Searching...
Jumapili, 30 Juni 2013

CHELSEA WAONGEZA DAU KWA CAVAN,ARSENAL WAONGEZA DAU KWA ROONEY PIA WANAMTAKA TORRES

 Wanted man: Edinson Cavani is a target for Chelsea and Real Madrid
EDINSON CAVAN.
Chelsea wamatuma ofa mpya ya paundi milioni 45 ili kufanikisha kumnasa mshambuliaji anayetikisa vigogo vya soka katika usajili ambaye kwa sasa ni mali halali ya Napoli Edinson Cavani -japo kiasi hicho kikubwa ya fedha bado kinaonekana kidogo kwani Napoli wanahitaji paundi milioni 52 ili kumuachia msukuma ndinga huyo raia wa Uruguai

Gunner be interest: Wayne Rooney's future remains in doubt
WAYNE ROONEY.
Klabu ya Arsenal katika kuonyesha kwamba imepania kukisuka kikosi chake upya sasa imempandia dau Wayne Rooney na kutuma ofa ya paundi milioni 20 ili kuwashinikiza Man U kumuachia Rooney lakini bado ushindani kati ya Arsenal na Chelsea katika kumuwania Rooney unaonekana ni mkubwa kwani Chelsea nao wamesema watatuma ofa yao kwa Man U ofa ambayo ni kubwa kuliko ya Arsenal ili kumnasa mshambuliaji huyo raia wa England ambaye ni mmoja kati ya washambuliaji waliopo kwenye listi ya mreno Mourinyo katika ujio wake wa pili darajani akitokea Madrid,japo taarifa kutoka kwa uongozi wa Man U zinasema Rooney hauzwi kwa dau lolote
DAVID MOYES-KOCHA WA MAN U.
Fernando Torres of Chelsea shoots at goal
Fernando Torres akiifungia  Chelsea 
Kocha wa Arsenal  Arsene Wenger amesema sasa anataka kumleta mshambuliaji ambaye anaonekana kutokuwa katika mipango na kocha wake wa chelsea muhuspania Fernando Torres ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

JOSE MOURINHO
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema hana mpango wa kumtumia Torres katika kikosi chake msimu ujao na kumruhusu kutafuta timu anayoipenda kuchezea kabla Arsenal hawajaanza kumtolea macho,hata hivyo Mourinho amekwenda mbali zaidi na kusema pia mhispania Juan Mata na mbrazili David Luiz nao pia hawamo katika mipango yake msimu ujao.

 Rallying cry: Villas-Boas says he wants to fulfil his lifetime ambition

ANDRE VILLAS-BOAZ.

Kocha wa Tottenham mreno Andre Villas-Boaz ameweka wazi kwamba ataachana na kufundisha soka baada ya miaka kumi ijayo na kujiunga na Dakar Ralley

AVB alianza kufundisha soka akiwa na umri wa miaka 21 na kuweka historia ya kuwa kocha mdogo kuchukua kombe la Europa akiwa na umri wa miaka 33 akiwa na klabu ya Porto

AVB akiwa na mwanaye.

katika harakati za usajili AVB tayari ameweka wazi kwamba yupo tayari kununua wachezaji wazuri ili kuimarisha kikosi chake msimu ujao ambapo tayari kuna habari kwamba amemnasa mbrazili Paulinho wiki chache zijazo.

POULINHO AKIWA NA TIMU YAKE YA TAIFA.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!