Mchezaji wa
klabu ya Manchester
City na timu ya taifa ya Ivory coast Yaya Toure amezungumzia masikitiko
yake kufuatia kifo cha kaka yake Ibrahim Toure na kuishutumu timu yake
kwamba walimnyima ruhusa ya siku nne kwenda kumuuguza marehemu kaka yake
kitendo ambacho amesema hatakaa akakisahau maishane mwake.
Marehemu Ibrahim Toure enzi za uhai wake akiwa uwanjani wakati anaichezea timu ya Beirut mwezi wa kumi mwaka jana. Ibrahimu alifariki dunia huko jijini Manchester alipokuwa anapatiwa matibabu ya saratani, Ibrahim amefariki akiwa na miaka 28
Yaya Toure na kaka yake Kolo Toure wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mechi yao ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya Japan mapema mwezi huu.
Kwa kauli hii ya Toure kwamba Man City walimnyima ruhusa kwenda kumona kaka yake wakati anaumwa inatarajiwa kuzua utata mkubwa klabuni hapo zaidi ya ile aliyowahi kuitoa hapo awali kwamba timu yake haikumpa sapoti katika sikukuu yake ya kuzaliwa na walimnyima keki. Huenda Toure akaihama timu hiyo msimu ujao kutokana na kauli zake tata.
0 comments:
Chapisha Maoni