Baada ya tukio la kushtua la jana usiku la mchezaji wa Uruguay kumng'ata beki wa Italia Giorgio Chiellini makubwa yameibuka kwamba kumbe alijaribu kumng'ata katika Chiellini mwaka jana katika michuano ya kombe la Confederations lakini jaribio lake likashindwa kama picha zinavyoonyesha.
Hapa alikua anaendelea kumsogelea karibu huku akiwa ameandaa meno mithili ya simba mwenye njaa lakini alikwaa kisiki mwaka jana.
Baada ya Chiellini kugundua mpango wa Suarez wa kumla nyama mbichi ndipo amlipomgeukia na kutaka kumpa ngumi za kutosha lakini akakumbuka kwamba masumbwi hayaruhusiwi uwanja wa mpira wa miguu.
Wahenga walisema Subira yavuta heri,hatimaye baada ya jaribio la Luis Suarez la kumla nyama na kunywa damu ya Girogio Chiellini alivuta subira na hatimaye Mungu sio Athumani wakapangwa kundi moja na ndipo alipohakikisha kwamba anatimiza ndoto yake ya kumla muitaliano bila huruma. shoulder during Uruguay's win over Italy.
wataalamu wa mambo ya kidunia wanahusisha tukio hili la Suarez kumng'a mwenzake kama tukio la kishirikina na inaelezwa pia kwamba mafanikio makubwa ya Suarez yanatokana na ushirikina.
Giorgio Chiellini aking'aka kwa mwamuzi huku akimuonyesha lama ya meno ya Suarez kunako begani mwake.
Hili ni tukio la tatu kwa Luis Suarez kuwang'ata wachezaji wenzake uwanjani ambapo tukio la kwanza alimg'ata mchezaji wa PSV Ottman Bakkal akicheza dhidi ya mwaka 2010, la pili alimg'ata mchezaji wa Chelsea beki Branislav Ivanovic 2013, na la tatu sasa ni la beki wa Italia hapo jana.
Huyu hapa Ottman Bakkal mchezaji wa PSV akionyesha jeraha la meno ya Suarez
Hapa Luis Suarez akimg'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic mwezi April 2013
Ikumbukwe kwamba baada ya kumng'ayta Ivanovic Luiz Suarez alifungiwa mechi kumi...sasa tusubiri tuone kwa tukio hili FIFA watampa adhabu ganiiiiiiii?????? au atasamehewaa????
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Chapisha Maoni