Malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose) ya Filipe Henriques kutoka Guinea Bissau ADY de Batista akiwasili huku akiongozana na Meneja wake Sholey Maqueta kwenye usiku maalum wa tuzo wakati wa tamasha la 17 la ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar kwenye viunga vya Ngome Kongwe
Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar, Bw. Samuel(kulia) Bond na Mkewe Jenny Bond wakibadilishana mawazo na mmoja wa majaji wa tuzo za ZIFF…
Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar, Bw. Samuel(kulia) Bond na Mkewe Jenny Bond wakibadilishana mawazo na mmoja wa majaji wa tuzo za ZIFF 2014 Mykel Parish (aliyeipa mgongo kamera) kabla ya kuanza kwa tuzo za ZIFF 2014.
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akiwakaribisha wageni waalikwa waliohudhuria usiku maalum wa tuzo za tamasha la 17 la ZIFF 2014 zilizofanyika mwishoni mwa juma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Bw. Richard Bell akizungumza na wageni waalikwa wakati utoaji tuzo za ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar. Aidha mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku itaendelea kuhakikisha inasaidia kuinua kiwango cha uigizaji na utengenezaji sinema za Kiswahili kwa kutambua kwamba filamu hizo ni sehemu ya uzalishaji wa fedha katika taifa kupitia utamaduni na kutoa wito kwa wasanii wa Bongo Movie kupeleka kazi zao kwa ajili ya kuonyeshwa kwenye chaneli za ving'amuzi vya ZUKU na kujitangaza kimataifa kupitia ving'amuzi hivyo.
Mmoja wa majaji wa tuzo za Signs kwenye tamasha la ZIFF 2014, Adinda Pamela akitangaza washindi wa tuzo hizo. Katikati ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na kulia ni mmoja wa "ushers" akiwa ameshikilia tuzo hiyo.
Mmoja wa washindi wa tuzo za Signis alikuwa ni ADY de Batista malkia wa Filamu ya Espinho da Rosa (the Thorn of the rose). Pichani ni ADY de Batista akisindikizwa jukwaani kupokea tuzo na Meneja wake.
Mmoja wa majaji wa tuzo za Signis Adinda Pamela akimpongeza ADY de Batista baada ya kunyakua tuzo hizo.
ADY de Batista akiongea kwa furaha kwenye usiku maalum wa tuzo za Signis katika kusheherekea tamasha la 17 la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar.
Channel Coordinator wa ZUKU Swahili, Bilha Olimba akitangaza jina la mshindi wa tuzo za ZUKU PEOPLE's CHOICE. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford akielekea jukwaani kumchukulia msanii mwezake Jacob Steven almaarufu kama JB alitwaa tuzo ya ZUKU PEOPLE'S CHOICE kupitia filamu yake ya SHIKAMOO MZEE kwenye tamasha la 17 la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akikabidhi tuzo ya ZUKU PEOPLE's CHOICE kupitia filamu ya SHIKAMOO MZEE ya mwigizaji Jacob Steven almaarufu kama JB iliyopokelewa na msanii mwenzake Shamsa Ford.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akimkabidhi tuzo mwigizaji bora Jackson Laurent Kabirigi kupitia filamu ya "Kisate na Nguvu ya Imani" (wa pili kushoto) aliyeambatana na ndugu yake Feysal Arikardy (kushoto).
Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, William Mtitu akielekea jukwaani kumpokelea tuzo mwongozaji wa filamu Issa Mussa a.k.a Cloud 112 aliyetwaa tuzo ya uongozaji bora kupitia filamu yake ya SHAHADA ndani ya tamasha la 17 la ZIFF 2014.
FILAMU ya Espinho da Rosa
(the Thorn of the rose) ya Filipe Henriques kutoka Guinea Bissau
imeondoka na tuzo tatu katika tamasha la 17 la filamu la kimataifa la
Zanzibar (ZIFF).Tuzo hizo ni pamoja na ya Signis , tuzo ya majaji na
tuzo ya fedha ya ZIFF.
Katika tamasha hilo filamu iliyotwaa tuzo
ya dhahabu ni ile ambayo ilikataliwa kuoneshwa nchini Nigeria
ilikotengenezwa ya Half of a Yellow Sun iliyoongozwa na Biyi Bandele.
Shughuli za utoaji tuzo ambazo
zilitanguliwa na hotuba ya makamu mwenyekiti wa kampuni ya wananchi
Group ambayo brand yake ya zuku ndio inafadhili ZIFF pamoja na tuzo zake
za Swahili, zilinogezshwa na vikundi mbalimnbali kikiwemo cha
kereografu cha B 6.
Aidha mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku
itaendelea kuhakikisha inasaidia kuinua kiwango cha uigizaji na
utengenezaji sinema za Kiswahili kwa kutambua kwamba filamu hizo ni
sehemu ya uzalishaji wa fedha katika taifa kupitia utamaduni.
Aidha alisema pamoja na mamilioni ya
shilingi walioyoahidi kutumbukiza katika miaka 10 ni vyema taasisi
nyingine hasa za umma kutambua uwapo wa tamasha hilo ambalo likitumika
vyema ni chanzo kikuu cha fedha kwa serikali na watu wake.
Katika utoaji wa tuzo ambao ulionekana nchi ya Afrika Kusini kufanya vyema, mtendaji wa ZIFF Professor Martin Mhando alizungumza maana ya nchi za majahazi na nini kinastahili kufanywa.
Katika utoaji wa tuzo ambao ulionekana nchi ya Afrika Kusini kufanya vyema, mtendaji wa ZIFF Professor Martin Mhando alizungumza maana ya nchi za majahazi na nini kinastahili kufanywa.
via Globa publishers.
0 comments:
Chapisha Maoni