ROBIN VAN PERSIE.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi ambaye kwa sasa anakipiga na Manchester United ambao wanaonekana kupoteza mwelekeo Robin van Persie, 30, amesema anatarajia kurejea katika kikosi chake cha zamani cha Arsenal mwishoni mwa msimu huu kufuatia mahusiano mabovu na kocha wake Moyes,huku akiweka wazi kwamba alitua Man U kwasababu ya kocha wake aliyestaafu
Sir Alex Ferguson.
DAVID SILVA.
Miamba ya soka ya Hispania Barcelona wamesema wanataka kumsajili kiungo machachari wa Manchester City David Silva kwaajili ya kuziba pengo la nahodha wao Xavi mwenye umri wa miaka 34 ambaye yupo mbioni kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu.
0 comments:
Chapisha Maoni