Searching...
Jumatatu, 3 Februari 2014

ANGALIA MATUKIO YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM KATIKA PICHA

 Hii ndiyo CCM, Rais Jakaya Kikwete akisema, huku akionyesha alama ya CCM ya jembe na nyundo ambayo aliichukua kwa mmoja wa mashabiki wa CCM walioingia nayo Uwanjani 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kuwaongoza wana-CCM katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya CCM 
 
 Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi waliofurika katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya alipoingia Uwanjani hapo huku akiwa na Mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa CCM, Abdurlahman Kinana
Vijana wa CCM wakicheza gwaride la ukakamavu mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete wakati wa sherehe hizo.
 Vijana wa CCM wakicheza halaiki
 Vijana wa Umri wa miaka 37, wakirusha njiwa hewani kila mmoja, kuashiria CCM ilivyofanikiwa kujenga amani na utulivu Tanzania katika uhai wake wa miaka 37 hadi sasa, wakati wa sherehe hizo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Kikwete kuhutubia hadhara
 Rais Jakaya Kikwete akihutubia
 Wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya waliojiunga na CCM,wakishangilia baada ya kutambulishwa na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye kwenye sherehe hizo
Msanii wa filam, JB akizungumza baada ya yeye na wenzake kukaribishwa na Nape
 Wasanii wa Filam na muziki wa kizazi kipya wakiselebuka baada ya kutangazwa kuwa watapewa kadi za CCM na Mwenyekiti wa CCM, Rais jakaya Kikwete kwenye sherehe hizo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiungana na wasanii waliokuwa wakicheza ngoma ya kinyakyusa wakati wa sherehe hizo
 Nape na Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda wakicheza muziki wa hamasa uliokuwa unapigwa na TOT wakati wa sherehe hizo.
 Khahija Kopa akituzwa na mashabiki alipotumbuiza katika sherehe hiyo akiwa na TOT
Kinana akisoma toleo maalum la gazeti la Mzalendo wakati akiwa kwenye sherehe hizo
 Ofisa wa Uhuru Publications Limited, akiwagawia wasanii magazeti ya Mzalendo
 Wasanii wakisoma Mzalendo
 Wasanii wakisoma gazeti la Mzalendo
Banda la UHURU/Mzalendo katika viwanja vya Sokoine mjini Mbeya

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!