Searching...
Jumatatu, 13 Januari 2014

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATATU JAN.13,2013

 JUAN MATA.
Timu ya Bayern Munich ipo katika mbio za kumuwania kiungo mshambuliaji wa Chelsea ambaye kwa sasa anaonekana kutupiwa virago na timu yake ya Chelsea Juan Mata,25,japo kuwa itabidi kufanya kazi ya ziada kwani vilabu vya  Paris St-Germain na Napoli wapo katika vita ya kuwania saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania. 
 
YOHANA CABAYE.
Arsenal wameweka wazi mipango yao ya kumuwania kiungo wa Newcastle Yohana Cabaye 27, na beki kisiki wa wa timu Davide Santon 23 kwa kitita cha paundi milioni 30. 
 
KEVIN DE BRUYNE.
Mkurugenzi wa michezo wa timu ya Wolfsburg Klaus Allofs ana uhakika kwamba ndani ya siku chache zijazo watamsajili kiungo wa Chelsea Kevin de Bruyne, 22.  
KURT ZOUMA.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anataka kumsajili beki kinda wa miaka 19 anayekipiga na timu ya St Etienne Kurt Zouma kama mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo kwaajili ya kuja kuchukua mikoba ya nahodha wa timu hiyo John Terry. 
 
 SAUL NIGUEZ.
Manchester United wameungana na Arsenal pamoja na Chelsea katika vita ya kuwania saini ya kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez, ambapo tayari kocha msaidizi Phil Neville amekwea pipa hadi Hispania kufuatilia kwa karibu uwezo wa kinda huyo wa miaka 19.  
 
JOLEON LESCOTT.
West Ham wamekubali kumsajili kwa mkopo beki wa Manchester City Joleon Lescott, 31, na kumlipa kitita cha paundi 90,000 kwa wiki kwa makubaliano kwamba watamsajili jumla kwa mkataba wa miaka mitatu endapo tu timu hiyo itaweza kusalia katika ligi kuu England msimu ujao.  
PATRICE EVRA.
beki wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga kwa sasa na timu ya Manchester United Patrice Evra, 32, ameweka wazi kwamba ataondoka Manchester United mwezi wa sita mwaka huu pale mkataba wake utakapokwisha. .

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!