
Nimekuiteni hapa kutoa salamu zangu za mwaka mpya kwa kuzungumza nanyi juu ya mustakabali wa mambo na hasa haya ambayo yanaendelea kujiri katika duru za kisiasa katika nchi yetu.
Bila ya kumung’unya maneno ni kweli ...........
kwamba hivi sasa taifa lipo katika hatua kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka ujao.
Ndugu zangu Wanahabari,
Martin Luther King,Junior aliyezaliwa 1929 na kufariki mwaka 1968 aliwahi kusema na
hapa naomba nimnukuu,” Kwamba watu dhaifu huisubiri fursa lakini watu makini huzifuata fursa,”.
Vivyo hivyo kwa mwanafalsafa mwenzake wa Kigiriki, (Plato 427-347 BC), aliwahi kusema pia, watu wema hawahitaji sheria kuambiwa namna ya kuwajibika lakini watu wabaya wapo radhi kutafuta kila aina ya njia kudidimiza fikra zako kwa kutumia nafasi aliyonayo,”… Hakika watu hao tunao na wanaonekana hadharani wakisaka kila namna ya udhaifu wa kibinadamu ili tuu, kufifisha ndoto za wenzao na hasa wenzetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hivi karibuni,tumesikia katika vyombo vya habari kwamba Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametangaza rasmi kuanza kwa safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake; akisema anataka kutimiza ndoto za watanzania wenzake za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Amekiri hadharani tena katika madhabahu kwamba anapowatazama marafiki zake wanaomuunga mkono, machozi yanamtoka na kwa uwezo wa Mungu atashinda kwani watanzania wanajua nia na ndoto yake.
Kwa umri wangu na kwa namna ninavyoitazama siasa ya Tanzania hivi sasa, Lowassa hakupaswa kushambuliwa na akina Nape Nauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa) na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa,mzee Philip Mangula kwa sababu moyo wake ulimruhusu kufanya hivyo,mbele ya mimbari ya Mungu na kwa namna ya pekee, hakutamka suala la kugombea urais.
The best way to predict the future is to invent it. Na kwa mantiki hiyo,njia sahihi aliyoitumia Edward Lowasa ya kutamka hadharani kusudio la kukamilisha majaliwa ya ndoto zake ni namna alivyonyambulisha kile kinachoshabihi mawazo yake ya muda mrefu ya kuwatumikia watanzania wenzake. Na hili si kosa ila ni msingi wa mawazo yake.
Ndugu zangu Wanahabari,
Haijalishi kwamba mimi ni mpinzani wa CCM na hata wao wanalijua hilo kwamba Ndesamburo ni nguli wa siasa za mageuzi ya kifikra katika nchi yetu lakini nasema kumshambulia Lowasa peke yake, ingali kunao vinara wengine wanaokigawa chama chao kwa kupita huko huko makanisani na misikitini kwa kisingizio cha kualikwa katika harambee,ni kuonyesha dhahiri chuki yao kisiasa dhidi ya Lowassa.
Nakuombeni watanzania wenzangu tuwakatae watu wanaotaka kutuchagulia viongozi wa kutuongoza.Tuwasikilize watu hoja zao na tutafakari kama kweli wanafaa kutuongoza.
0 comments:
Chapisha Maoni