Baada ya kutwaa taji alilokuwa akiliota miaka nenda miaka rudi la mchezaji bora wa dunia, mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema jana usiku kwamba anakaribia kurejea nyumbani Manchester United msimu ujao.
Cristian Ronaldo amekuwa akihusishwa mara kwa mara kurejea ligi kuu England kunako Old Trafford sasa amekoleza moto huo kwa kusema msimu ujao atarudi nyumbani
‘Ni kweli nilizungumza na Rio Ferdinand kuhusu kurejea Man U msimu ujao,’ alisema Ronaldo.
‘Rio ni mtu makini sana na amejitahidi mara kwa mara kubadili mawazo yangu kuhusu kurejea manchester United.
‘Nimefikiria mara kwa mara kuhusu United. bado wapo moyoni mwangu na ndiyo timu niliyoichezea miaka minne. Naipenda sana timu hii.
0 comments:
Chapisha Maoni