DIEGO COSTA.
KLABU za Chelsea na Atletico Madrid
zimekubaliana kubadilishana wachezaji, Diego Costa ahamie Stamford
Bridge msimu ujao, kwa mujibu wa vyombo habari Hispania.
Kipa wa Blues, Thibaut Courtois,
anayecheza kwa mkopo Atletico, amekuwa akizungumziwa na wengi kama
mlinda mlango hodari kinda Ulaya, baada ya kudaka vizuri akiwa na klabu
hiyo ya Hispania kwa misimu mitatu.
THIBAUT COURTOIS.
Lakini kipa huyo mwenye umri wa miaka
21 angependa kubaki Madrid, na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anamtaka
mshambuliaji nyota, Costa arejee. Kocha wa Manchester United, David
Moyes alitumai kumpata mshambuliaji huyo Old Trafford.
Costa amefunga mabao 19 katika La Liga msimu huu, akishika nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Cristiano Ronaldo wa Real.
JOSE MOURINHO.
Kipaumbele cha Mourinho katika usajili huu ni mshambuliaji, na Mreno huyo amegoma kuondoka Januari.
Chelsea ilitaka kipa Courtois asaini Mkataba mpya licha ya kwamba hajawahi kuchezea timu ya Stamford Bridge, lakini Mbelgiji huyo angependa kuchezea klabu kwa Mkataba wa kudumu badala ya mkopo.
Courtois awali alisema atarejea Chelsea tu kuwa kipa namba moja mbele ya Petr Cech.

0 comments:
Chapisha Maoni