Mkuu wa Kanisa Katoliki, Baba Mtakatifu Francis,
ametoa wito kwa Wakristo wote kote duniani kufungua nyoyo zao na kupambana na nguvu za
giza.
Akiendesha misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro,
ambayo ni ya kwanza kwake tangu kuchaguliwa kuongoza kanisa hilo lenye
wafuasi bilioni 1.2 duniani, Baba Mtakatifu Francis amesema Wakristo
hawapaswi kuachia ubinafsi kuyaongoza maisha yao.
"Mungu ni nuru, na kwake hakuna giza lolote", alisema Papa Francis
akinukuu kitabu cha Injili ya Mtakatifu Yahya, akiwasifu wachunga kondoo
wa Uzawa, ambao alisema ni watu pekee walioshuhudia kuzaliwa kwa Yesu
Kristo mjini Bethlehem "kwa kuwa walikuwa ni watu wa mwisho, masikini
wanaotengwa."
Papa huyo mwenye asili ya Argentina na ambaye amewavutia wengi kama
mwanaharakati wa haki za wanyonge tangu kuchukua nafasi ya mtangulizi
wake, Mjerumani Benedict wa 16 mapema mwaka huu, alitoa wito kwa waumini
wa Kikristo kupambana na udanganyifu, ufahari na ubinafsi, ambavyo kwa
pamoja aliviita roho ya giza.
0 comments:
Chapisha Maoni