KLABU ya Arsenal imepangwa na wapinzani wao wa London Kaskazini, Tottenham katika Raundi ya Tatu yaKombe la FA.
Manchester
City watasafiri kuifuata Blackburn Rovers, Chelsea watamenyana na Derby
ugenini na Manchester United watakuwa wenyeji wa Swansea.
Mabingwa wa sasa, Wigan wataanza kampeni zao za kutetea taji kwa kumenyana na Milton Keynes Dons nyumbani.
Wigan ilishinda Kombe la FA msimu uliopita baada ya kuifunga Man City katika fainali
Aidha,
Liverpool itamenyana na Oldham au Mansfield Uwanja wa Anfield, wakati
West Brom itacheza na Crystal Palace, Newcastle na Cardiff na Norwich na
Fulham.
Oldham
iliifunga The Reds 3-2 katika Raundi ya Nne mara ya mwisho na
watakutana na kikosi cha Brendan Rodgers kama wataitoa Mansfield katika
mchezo wao wa marudiano wa Raundi ya Pili.
Liverpool pia ilikutana na Mansfield katika Raundi ya Tatu msimu uliopita, na Luis Suarez aliiongoza timu yake kushinda 2-1.
Luis Suarez aliisaidia Liverpool kuitoa Mansfield
Mara
ya mwisho Arsenal kushinda Kombe la FA ilikuwa mwaka 2005, lakini ili
kushinda taji hilo tena italazimika kuwafunga wapinzani wake wakuu.

0 comments:
Chapisha Maoni