RAIS WA KENYA BWANA UHURU KENYATA.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amevunja ziara yake ya kushiriki
kwenye hafla ya kuwakabidhi Wakenya wenye asili ya Kinubi hati za
kumiliki vibanda vyao kwenye eneo la mabanda la Kibera la mjini Nairobi
kwa sababu za kiusalama.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, washauri wa Kenyatta wamemshauri
asihudhurie hafla hiyo iliyoitishwa na Waziri wa Ardhi wa Kenya Bi
Charity Ngilu kwa sababu jambo hilo limelalamikiwa na wakazi wa Kibera.
Huku hayo yakiripotiwa, habari kutoka mjini Nairobi zinasema kuwa,
hafla ya kukabidhi hati miliki iliyokuwa imepangwa kufanyika leo huko
Kibera, imevunjwa.
WAKAZI WA KIBERA NCHINI KENYA WAKATI WA UCHAGUZI ULIOPITA.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamelalamika kuwa wamedharauliwa katika suala hilo na wametishia kuvunja usalama wa eneo hilo.
Hata hivyo msemaji wa Rais Kenyatta, Manoah Esipusu amesema kuwa
Kenyatta hakuwa amepanga kushiriki kwenye hafla hiyo na wala ziara hiyo
haikuwemo kwenye ratiba zake za leo.
0 comments:
Chapisha Maoni