Searching...
Jumatano, 25 Desemba 2013

MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA KIROHO KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI SOLLY MAHLANGU KUWASHA MOTO UWANJA WA TAIFA LEO

 Mwanamzuki mwimbaji  wa Kimataifa wa nyimbo za Kiroho  kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu pichani kati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili jana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar  .Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza leo kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krisimasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kuhusiana na ujio wa mwanamuziki wa Afrika Kusini,Solly Mahlangu aliyewasili jana jioni jijini Dar se salaam tayari kuungana na wanamuziki wengine wa nyimbo za Injili kwa ajili ya kutumbuiza leo kwenye tamasha la Krisimasi,ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili,Solly Mahlangu akiwapungia mikono mashabiki wake waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili jana jioni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza leo kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!